Tuesday, May 31, 2011

ALIOKWAMBIA ULAYA HAKUNA WAUZAJI WA VITUMBUA NANI?

Katika pita pita zangu week end mitaa ya stockholm  nikakuta sehem vibanda vingi na kila kibanda kina biashara zake, ila nilivutiwa na kibanda hiki na nikasogea karibu kutazama nikagundua kinachopikwa hapa ni vitumbua ila tofauti inaonekana katika vifaa ila wanageuza na kuweka mafuta kama vile anavyopikaga mama vyakuuza kule Tanzania.

HIZI SIO MILA NA DESTULI ZETU WATANZANIA JAMANI TUNAELEKEA WAPI?

 Akina dada wakilishana keki kwa kutumia midomo,jamani ndio uzungu au utandawazi?kipindi cha mwalimu nyerere hawa ni viboko kwa kwenda mbele.
 Haya muoneni Lulu nae mhh.Hvi kivazi kama hiki kweli unakivaa mbele ya baba yako inawezekana?ndo mwanzo wa baba kula kuku na mayai yake.

Wewe Lulu na hivi vinguo unavitoaga wapi?na bora unavyoishia kupiga navyo picha na kwenda navyo club,ebu jaribu siku moja kukatiza mtaa wa kongo na kivazi hichi nadhani hutorudia tena katika maisha yako. 
Jamani tunapotea jamani ndo nini hivi ebu wadau tusaidiane kweli watu wa jinsia moja wanashikana shikana kama hivi jamani?

Sunday, May 29, 2011

MIONGONI MWA MASHABIKI WA MANCHESTER AMBAO KIPIGO KILIWAHUSU.

 Pole sana ndugu mgiriki najua kipigo jana kimekufanya hata chakula kisipite.
 Huyu ndugu yangu Mweneu kiukweli mkiwa mnatazama mpira wala hujui kama anapenda Manchester au la ila jibu upatikana baada ya mechi kuisha na kupata ushindi,huwa na furaha sana ila jana alikumbwa na hasira mpaka akawa anatukana wachezaji hawachezi vile inavyotakiwa wewe ukipewa nafasi utacheza kaka?Pole sana ndugu yangu Mweneu ndo mpira jifute machozi na kombe la league ya england.
 Shekhan Rashid sijui jana ulikua katika hali gani maana manchester wakifungwa uzimaga simu vipi jana kaka?
 Mimi jana kiukweli kipigo hakikunistua sana sababu naujua mpira wa fainal una matokeo mawili na si matatu kufungwa au kufunga.Sema huyu jamaa wa katikati Herry najua jana yeye alikua na homa kali sana je ulimeza panadol kaka?kwa upande wa Cledo mwaipopo najua alikua na furaha yeye ni mzee wa bwawa la maini najua jana alikua Barchelona.

Hahahahaha huyu kipa wetu wa kutumainiwa wa kilimanjarofc hapa stockholm Kablau hua anaongea maneno yote Manchester wanaposhinda sasa jana ilikuaje ndugu?pole ndugu najua ulitamani ungedaka wewe jana ila Mesi popote anashinda.

Saturday, May 28, 2011

BARCHELONA MABINGWA KLABU BINGWA ULAYA 2011

 Kiukweli asiekubali kushinda siku zote si mshindani na ukweli usiofichika jamaa wamecheza mpira wa hali ya juu sana,hakuna chochote chakusingizia ongera sana Barca.
 Van der sar akiruka bila mafanikio na mpira kutinga wavuni.
 Katika kitu kisichofichika katika ulimwengu wa mpira huyu mtoto anafaa kuogopwa hata kuliko simba,kwani anaweza kufanya lolote anapokua uwanjani na ndio alichokifanya leo.
 Wayne Rooney akijaribu kuipa uhai manchester united kwa kusawazisha goli lakini mambo hayakua kama alivyotegemea na matokeo yake mpaka mechi inakwisha uzuni ulikwenda old trafford.
Poleni sana team nzima ya manchester na mashabiki wake ndio mpira.

Friday, May 27, 2011

DAKIKA 90 NDIO ZITAIPA MANCHESTER UNITED AU BARCELONA FURAHA

Siku ya leo dunia nzima ifikapo sa tatu kasoro ya usiku kila mmoja macho yake yatakua katika luninga kutazama fainali ya klabu bingwa ulaya kati ya Barcelona na Manchester United.Najua mashabiki wa pande zote wanahitaji kupata furaha kwa kuchukua kombe hilo,ila ukweli unabaki pale pale anatakiwa kupatikana mshindi na mshindwa.Najua mashabiki wakubwa wa manchester kama Kablau,Mkangwa,Mgiriki,Herry,Shekhan,Ahmed Nayal,Abdallah Ramadhani,Iddi Harambe,Kibabu woote wanalingoja kombe kwa hamu kubwa ila dakika 90 ndio zitatoa matokeo.
 Blog yako itakuletea picha zote za mechi hiyo baada ya kuisha.

WATU WENGI WANAJIULIZA KUZAA KWA IRENE UWOYA NDO MWISHO WA UJANA WAKE?

 Hapo irene enzi zake kabla ajaolewa .

Sasa hivi Irene anaitwa mama flani watu wanajiuliza ndio mwisho wa makeke yake au ndio ikipita arobaini mwendo mdundo?

WATOTO WA MJINI TWANGA PEPETA WALIVYOKAMUA BILLICANAS JUMATANO ILIOPITA.

 Hapa naona kikosi kizima cha akina dada wa twanga pepeta wakisugua kisigino hii style inanimaliza sana.
 Kama kawaida wakiwajibika kazini vijana wa twanga a.k.a watoto wa dar.
 Mashabiki nao hawakua nyuma kuakikisha wanakwenda sawa  naona full kujiachia.
Ebwana huyu anaitwa charlz baba a.k.a jembeeeeeee la twanga anajua sana huyu mtu ukitaka kuamini msikilize katika nyimbo ya mwana dar es salaam utakubali maneno yangu.Pia namkubali anaenda nayo sawa kazi yake akiwa jukwaani kwani muda wote upendeza kama hivi.
Picha kwa hisani ya kingkif.

Wednesday, May 25, 2011

MZEE WA MBAGALA HUYOOO NDANI YA SWEDEN

East African Superstar Diamond Platnumz will be touring Europe in the month of June. He will be performing for the first time in Sweden, Norway, Holland, Belgium among other countries in the region. The tour begins on the 10th and ends on the 19th of June.Enjoy your 2011 Summer in Europe with Diamond .
   Habari zaidi siku na tarehe atakayotoa burudani mtajulishwa.

UKIONDOA UNAZI JAMAA NAMKUBALI SANA.

Team capten wa bwawa la maini Steven Gerrard akuna asiyemkubali hata kama si mpenzi wa bwawa la maini,akiwa uwanjani anaweza fanya lolote na muda wowote.

Patrice Evra has suggested that fellow Frenchman Samir Nasri should join Manchester United if he wants to win trophies.

Sasa patrik evra unatafuta ugomvi na watu wa Arsenal,yaani huyu wanavyomtegemea unamshauli aende manchester!!

Atletico Madrid president Enrique Cerezo says he is waiting to be informed of Manchester United's likely signing of goalkeeper David De Gea.

Dah bora uje kuziba pengo la van der sar.Maana hao akina drogba,suarez na samir nasri wanavyotaka sifa tutaangukia pua.

Tuesday, May 24, 2011

HAWA ORIJINO KOMEDI NAWAKUBALI SANA TAZAMA HII

HVI KWELI HOME BOY WANGU UNATAKA KUUZA UHAI WAKO KWA BAISKELI?

 Unajua nilipotazama picha ya kwanza nikahisi kama jamaa namjua,nilipoendelea kutazama zaidi nikazidi kukubaliana na kichwa changu.Na niliposoma jina lake ndio uhakiki wangu ukatimia na kuanza kupatwa na huzuni mkubwa.Kwa ufupi jamaa namjua tunaishi nae mtaa kimoja temeke na alikua golikipa wetu mzuri sana mpira wa makalatasi kipindi wadogo.Sema bdae nilipokwenda bongo nikakuta ameanza kutumia madawa ya kulevya,nikajua mwisho wake unaweza kufikia huku siku moja.Mimi sina zaidi ya kusema kumuombea mungu ajijue yeye nani na anathamani gani kama binadam asiuchezee uhai wake.

 Dah tazama hapa wanavyomgombania kama mpira wa kona.

 Huyu askari na jamaa aliovaa shati jeupe ndio waliomnusuru la sivyo yangekua mengine.


 Jitambue ndugu yangu usije ukakukuta umauti wako kwa sababu ya vitu vidogo.

Hili guu la jamaa sidhani kama lilimkosa.Hili tukio lilitokea morogoro nadhani mjomba Jamil na Abui mtakua mnapajua haya maeneo.

Monday, May 23, 2011

MASTAA WA BONGO MOVIE NDANI YA JIJI LA MWANZA KTK MECHI YAKIRAFIKI

 Kikosi kizima cha bongo movie wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mechi.
 Hapa naona kikosi kizima cha netball cha wanadada wa bongo movie wakipata picha ya pamoja wakiongozwa na capten wao Jackline Wolper.
 Wema Sepetu nae ndani ya mwanza akijumuika na wenzie wa bongo movie,pembeni namuona capten wa netball ya bongo movie Jackline Wolper.
 Steve Nyerere na Wema Sepetu wakipata kinywaji taratibu.
 The greatest Ray na Jackline Wolper wakibadilishana mawazo
 Wana bongo movie wakiwa ndani ya basi.
Hisani Muya au Tino jina la kisanii akiwa na mrembo wa bongo movie.
Picha kwa hisani ya Ray the greatest.

Sunday, May 22, 2011

KATIKATI YA JIJI LA STOCKHOLM LEO JUMAPILI

 Hili eneo upendwa na watu wengi sana kupumzika na hasa kipindi hiki cha jua,
Daaah hivi vibanda vipi tena ndugu?au ndio wamachinga wa karume wameamia stockholm?

STOCKHOLM


Maeneo ya central station  stockholm watu kibao na mizunguko yao,naona hapo kina mtu na lake.