Saturday, October 29, 2011

NYIMBO YETU YA WEEK HII WADAU.VITUKO USWAHILINI-SUMA G

MAJAMBAZI TABATA WAMPIGA SHOKA LA KICHWA MLINZI HUYU NA KUGANDIA KICHWANI.

 Wadau picha hizi zinatisha lakini mtuwie radhi kwani ndiyo hali halisi iliyotokea usiku wa kuamkia leo huko Tabata na hakuna mtu anayeweza kuvumilia maovu haya yanaofanywa na watu wasiokuwa na utu. Leo saa 12 asubuhi hospitali ya taifa Muhimbili imempokea mgonjwa anayeitwa Mussa Shabani(42) akiwa na shoka iliyonasa kichwani
(kama picha inavyooneka hapo chini).
Bwana Mussa ni mlinzi katika nyumba ya Joseph Mwakyusa huko Tabata. Majambazi yalipofika nyumbani kwa bawana
Mwakyusa yalimjeruhi
kwa shoka bwana mussa na, wakati majambazi yaliyovamia nyumba ya Mwakyusa yakiendelea kufungua spea za gari aina ya Toyota verosa. kwa bahati nzuri bwana Mwakyusa alishtuka
na ndipo
majambazi hayo yalipokimbia na kutoweka yakimuacha mussa katika hali mbaya na shoka ikiwa imenasa kichwani.
Madaktari wa taasisi ya tiba ya mifupa MOI walifanya kazi ya ziada kuitoa shoka hiyo na sasa Mussa yupo chumba cha wagonjwa
mahututi. bwana.
Jumaa Almasi afisa uhusiano mkuu wa MOI amethibitisha tukio hilo na kusema ''Ni kweli bwana Mussa amepokelewa hapa MOI akiwa na shoka iliyonasia
kichwani mwake lakini madaktari wamemfanyia upasuaji na kuitoa na sasa hivi yupo chumba cha wagonjwa mahututi''
Kiukwel inatisha sana hii hali ndugu zangu unataka kumoa uhai mwenzio kwa spea za gari!mungu amponyeshe haraka amen.Kwa hisani ya unique entertainment

Friday, October 28, 2011

KANUMBA NAE ANUNUA MKOKO MPYA WENYE THAMANI YA MILIONI 78

                          Ukiwa ndani unatazama orijino komedi bila chenga
 Katika kudhihilisha kwamba sanaa ya bongo inaelekea pazuri wasanii sasa wanakula jasholao kama hivi.

 Hapa Kanumba akiwa ameiegemea gari yake na kushow nayo love,babkubwa mzeya ulipotoka mbali kula matunda yako sasa.

Thursday, October 27, 2011

KAMA WEWE MNUNUAJI WA VITU DRJAYS.COM UJUE UNAGONGANA VIKUMBO NA MASTAA HAWA KTK KUNUNUA.

MKAZI WA KAWE JIJINI DAR AJINYONGA,SABABU NI MFARAKANO NA MKEWE

 Mkazi mmoja maeneo ya kawe jiji dar amekutwa chumbani kwake amejinyonga na kufa,mkazi huyo wa kawe ametambulika kwa jina la Barnabas habari za karibu zilielezwa jamaa alijinyonga kutokana na mifarakano na mkewe.

Hapa maiti ya bwana Barnabas ikiingizwa katika gari la polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi juu ya kifo chake.
   Habari kwa hisani ya unique entertainment.

SANAA BONGO INALIPA KWA SASA,TAZAMA MKOKO MPYA WA VINCENT KIGOSI A.K.A RAY





Tuesday, October 25, 2011

JUDITH SANGU AWA MISS KAMPALA INTERNATIONAL UNIVERSITY(KIU)

 Mshindi namba moja Judith Sangu  ndie alienyakua taji la mrembo wa chuo kikuu cha kampala internatinal university(KIU)





Monday, October 24, 2011

IJUMAA WAJA NA MPYA NYINGINE JUU YA DIMOND NA WEMA.


WEMA Isaac Sepetu, Jumatano iliyopita ilikuwa siku ngumu mno kwake na kama si jitihada za mzazi, leo yangekuwa yanazungumzwa mengine.

Wema ambaye hana historia ya kumlilia mwanaume, amekamatika kwenye penzi la brazameni anayedatisha ‘maduu’, Naseeb Abdul ‘Diamond’, Jumatano iliyopita baada ya kuambiwa anaachwa, aliona bora ajisalimishe kaburini kwa kunywa sumu.

Busara za mama mzazi wa Diamond, Sanura Khassim ‘Sandra’ ziliokoa jahazi kwa kumlazimisha mwanaye arudiane na Wema ili mambo yasiharibike.

WEMA ALIVYODATA
Jumatano iliyopita mchana, Wema alipata taarifa kuwa Diamond ‘Platinumz’ alishazungumza na waandishi wa habari na kuwaeleza uamuzi wake wa kumuacha jumla.

Wema ambaye ni Miss Tanzania 2006-07, alipata taarifa hizo akiwa kwenye kambi ya kurekodi filamu kwenye Hoteli ya Lamada, Ilala, Dar es Salaam.

Tukio la kwanza, Wema alivua pete ya uchumba aliyovalishwa na Diamond kwa hasira, akaanza kulia.
Baada ya kutafakari, Wema aliona mtetezi pekee ni mama mkwe wake, Sandra, hivyo alimpigia simu na kuangusha kilio cha “mama mkwe nisaidie mwanao asiniache.”

Utu uzima dawa, Sandra alimwita mrembo huyo nyumbani kwake, Sinza, Dar ili wazungumze. Mapenzi ya Diamond ndani ya Wema, yana nguvu kuliko kazi, kwa hiyo akaondoka kambini bila kurekodi na kumuacha prodyuza wa muvi hiyo, Suleiman Barafu akiwa na mshangao.

Barafu alikasirika lakini wasanii wenzake, walimshauri amvumilie Wema kwa sababu yupo kwenye mateso makubwa ya kimapenzi.
Wema alipofika nyumbani, alimvamia mama mkwe wake, ‘mchozi’ huo, akamlamba miguu, akasema: “Mama nampenda Diamond kuliko chochote, akiniacha sina pa’ kuweka sura yangu.”

Akamchanganya mama mkwe: “Sitanii mama, endapo Diamond ataniacha, sitakuwa na uwezo wa kubeba haya mapenzi makubwa niliyonayo. Nitakunywa sumu, nitakufa. Ila sitajali kwa sababu nitakufa kwa sababu ya penzi la mwanaume ninayempenda.”

Mama Diamond ‘Sandra’ kusikia hivyo, akapagawa: “Mkamwana afe juu ya nini?” Alimwita Diamond nyumbani wazungumze lakini muafaka haukupatikana.

KIKAO USIKU MZIMA TABATA
The Biggest IQ, Ijumaa Wikienda linajitosheleza kwa data kwamba Sandra alimlazimisha Diamond arudiane na Wema ili kuokoa uhai wa mrembo huyo.

Kwa Diamond, ilikuwa ngumu kukubali, akishusha madai kuwa Wema ni mvivu, hapiki chakula nyumbani, hafui nguo, kazi zote hizo zinafanywa na mama yake (Sandra). Ameshasikia mengi lakini siyo ishu, kubwa ni kwamba mrembo huyo anamlazimisha Platinumz amfukuze mama yake mzazi ili wawe huru.

Hata hivyo, mama mtu alipangua hoja za Diamond na kuwataka wamalize tofauti zao na kurudiana.
Kikao hakikuzaa matunda, saa sita usiku (Alhamisi), Diamond, mama yake, mjomba wake anayeitwa Saidi na kaka yake aliyefahamika kwa jina la Hamisi, walizungumza kwa muda mrefu kuhusu hatima ya mastaa hao.

BUSARA ZA KIUTU UZIMA
Habari zinasema kuwa baada ya mvutano wa muda mrefu, Saidi na Hamisi walisimama upande wa Sandra, hivyo kushinikiza Diamond kurudiana na Wema.
Kutokana na shinikizo hilo, Diamond alinywea, akasalimu amri mbele ya wakubwa.

WEMA KAFICHWA
Kumpata Wema kwa sasa ni kazi ngumu kuliko kumtafuta Mullah Omar, kwani simu yake imezimwa na vyanzo vyetu vimetutonya kuwa mrembo huyo amekatazwa na Diamond asizungumze chochote kwa rafiki zake wala kwa chombo chochote cha habari.

NENO LA DIAMOND
Gazeti hili lilizungumza na staa huyo Ijumaa akiwa Dodoma, alikokwenda kufanya shoo, hili ni jibu lake: “Ni kweli, mimi na Wema tumerudiana. Mama alishinikiza, kwa hiyo nikasalimu amri.”

KAULI YA FAMILIA
Mama wa Diamond hakupatikana lakini kaka yake, Hamisi alisema: “Dogo alikosea kumuacha mwenzake bila kumshirikisha mzazi wake.”

KWELI WEMA KANASA
Wema alishaachana na wanaume kadhaa ambao walibaki na sononeko, yeye hakujuta na alisonga mbele lakini kwa Diamond imekuwa tofauti.

Baadhi ya wanaume hao ni wasanii, Steven Charles Kanumba, Charles Gabriel Mbwana, Hartmann Osmund Mbilinyi na Jumbe Yusuf Jumbe.     



kwa hisani ya globalpublishers.

Saturday, October 22, 2011

WEEK TATU ZA KUVISHWA PETE YA UCHUMBA WEMA ABWAGWA NA DIMOND SABABU MAMA WA DIMOND

Msanii wa kizazi kipyaDimond amemtema rasmi mpenzi wake ambae ni msanii wa filamu za bongo Wema Sepetu.Habari zilizosibitishwa na waandishi wa habari ambazo walizipata moja kwa moja kwa mtu mzima Dimond,kweli kabisa ndugu waandishi nimeamua kuwaita na kuwaipa hii taarifa kwamba sipo tena na Wema japo nilimvisha pete week 3 zilizopita.Na sababu kubwa za kumuacha mrembo huyu ni kwamba ampendi mama yangu mzazi na hataki tukae nae pamoja anataka mama yangu nimrudishe tandale mm na yeye tuendelee kuishi Sinza.Kiukweli hili silikubali japo nampenda wema lakini mchezo na mama yangu mzazi sipo tayari kumtelekeza sababu ya mapenzi,kwani hata yeye Wema amesahau kwamba bila mama yangu yeye asingenijua,kwanza mama yangu amenizaa na amenilea kwa tabu baada ya baba yangu kunikataa nimepata shida na yeye mama yangu maisha yetu yote ya dhiki siku tunakula siku tunalala na njaa.Na huyo huyo mama yangu ndio niliomuibia pete yake ya dhahabu nikapata pesa na kwenda kurecord nyimbo na mama yangu akanivumilia na kunipa baraka na mpaka nikatoka katika mziki sasa huu ndio muda wake wakula tunda la mwanae mzeya sasa vipi nimtelekeze sababu ya yeye Wema?sipo tayari kwa hilo ni bora nimuache yeye sio mama yangu nadhani nimeeleweka waandishi.Wema nae alipotafutwa na kupatikana alishindwa kuongelea hili na kusema sipo tayari kuliongea hili sipo sawa kwa sasa nitawatafuta mwenyewe.

Friday, October 21, 2011

TAARIFA YA MSIBA

Feruzi Ahmed Said (Mume wa Dorina) amefiwa na baba yake mzazi Mzee Ahmed Said leo alfajiri.

Feruzi anapenda aende nyumbani (Dares Salaam) haraka iwezekanavyo kuhudhuria mazishi kama atawahi. Ikishindikana aende kuhani.

Yeye na mke wake wanaleta ombi la msaada wa hali na mali kwa jumuia ya watanzania ili Feruzi aweze kwenda katika mazishi.

Kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kumfikishia msaada huu kama una uwezo, tafadhali piga simu Na. 0722982865 (Feruzi) au 0737143048 (Dorina).

Kwa wale wataoweza kwenda kuwaona msiba uko, Konsolvägen 7, Hökarängen, (Green Line kwenda Farsta)

Watashukuru sana kwa msaada wenu.


KAMA KAWAIDA YETU MWENZETU ANAPOFIKWA NA TATIZO KAMA HILI NI WAJIBU WETU KUMKIMBILIA NA KUFARIJI,KWANI KESHO ITAKUA ZAMU YAKO WEWE AU MIMI PIA.TUNAOMBWA WOTE KWA PAMOJA TUPATAPO MUDA TUJITOKEZE NYUMBANI KWA MFIWA.

Thursday, October 20, 2011

MUAMMAR GADDAFI AULIWA KINYAMA

MLOPELO AILALAMIKIA CLOUDS FM KWA KUITUPA UVUNGUNI NYIMBO YAKE MSIKIE MWENYEWE.

Kwa jina anaitwa Khalid ni msanii wa maigizo alishawahi kuigiza kipindi cha nyuma akiwa na kundi la kaole,Jamaa ni mkazi wa temeke wailes,mimi kumbukumbu zangu toka nipo mdogo nimemkuta kama alivyo hivi.Siku za karibuni alitoa malalamiko yake katika media kwamba amepeleka nyimbo yake clouds fm na imewekwa kapuni haipigwi.

Monday, October 17, 2011

SIO KAZI PEKE YAKE NA MAPUMZIKO MUHIMU.MJERU AKIWA MAPUMZIKONI UJERUMANI

                                     Nakuonea gele mzazi kwa bata ulivyolila huko nchi za nje

                          Baba na mwana wakishow lv baada ya kutoonana kwa kipindi kidogo
                                    Furaha kwa kwenda mbele si unajua damu yako
                                                              A.k.a Rick Ro...........

                                                   Hapa hamza akiwa na ba mdogo

                                           Hahaha ebwana mtoto wa nyoka kweli nyoka



                              baba na mwana wakiwa katika mizunguko yao ndani ya jiji la munich
                                                                   Kikwangua anga

Baada ya bata leeeeeeefu sasa tunarejea kulikoungua shoka mpini ukabaki kuendeleza libeneke la kutafuta mawe.