Thursday, August 25, 2011

AMEKOSA NINI MALAIKA WA MUNGU HUYU MPAKA ATUPWE?

 Masikini malaika wa mungu amekosewa nini mpaka afupishiwe maisha yake?tena ni msafi hana hata kosa moja katika hii dunia.Naimani mwenyezi mungu atamuadhibu anayehusika.Kitoto kichanga kilikutwa kimetupwa katika mto na tayari ameshakufa.Kiukweli nilipokutana na habari hii mwili wangu ulisisimka sana na kujiuliza maswali mengi bila majibu juu ya tukio hili.Ila swali la mwisho ambalo ndio jibu nimekosa kabisa ikiwa wewe mwenyewe umekutana na mwanaume kwa raha zako na ukashika mimba miezi 9 jumlisha uchungu wa kuzaa kweli kabisa unamtupa mwanao uliompatia tabu?Kama maisha magumu huwezi kumuhudumia kwanini usiombe msaada kwa wasamalia wema?Hvi unadhani wanawake wenzake wale ambao mungu ajawajaalia kupata mtoto wala mimba kwa bahati mbaya wanamlaani vipi mwanamke aliofanya kitendo hichi cha kinyama?
Watu wakishuhudia tukio la kuokotwa kwa mtoto mchanga alietupwa katika mto na kukutwa amefariki.

KARIBU TUIAGE SUMMER KWA PAMOJA

END SUMMER IN STYLE BASKETBALL CUM NYAMA CHOMA FT TANZANIA,RWANDA,UGANDA VANUE SKOGÅS 5MINS WALK FROM STATION.AFTER PARTY....BEST  DJ´S BEN N WADADA SKY IS THE  LIMIT..27TH!!MEET ME AT VRETENSBORGSVÄGEN 21 IN HÄGASTEN FROM  22:00 TILL 05;00 HRS

Wednesday, August 24, 2011

MUALIKO WA FTARI KWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI SWEDEN

MUHESHIMIWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI SWEDEN ANAYO FURAHA KUWAALIKA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA KWENYE  FTARI SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 27.08.2011.MUDA NI SAA MOJA NA NUSU JIONI(19:30HRS )NYUMBANI KWA BALOZI VEDETVÄGEN 35 NÄSBY ALLE.MNAOMBWA KUFIKA WOTE KWA PAMOJA.
TAFADHALI MJULISHE NA MWINGINE UPATAPO TAARIFA HII.

Tuesday, August 23, 2011

TAARIFA YA KISOMO CHA KUMUOMBEA DUA BABA MKUBWA WA YUNUS.

NDUGU YUNUS WA KUNGSÄNGEN ANAWATAALIFU NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WA HAPA SWEDEN,KWAMBA SIKU YA IJUMAA 26.08.2011 SA MBILI KAMILI(20:00)JIONI NYUMBANI KWAKE KUNGSÄNGEN ATAFANYA KISOMO CHA KUMUOMBEA DUA BABA YAKE MKUBWA ALIEFARIKI TANZANIA SIKU YA JUMAPILI, NA KUZIKWA SIKU YA JUMANNE HUKO TANZANIA.
ANAWAOMBA WATANZANIA NA WASIO WATANZANIA KUHUDHULIA KATIKA KISOMO HICHO SIKU HIYO YA IJUMAA HAPO NYUMBANI KWAKE KUNGSÄNGEN,KUFIKA KWAKO WEWE NDIO UFANIKISHAJI WA KIMOSO HICHO.

UTARATIBU ULIOPANGWA NIKWAMBA WATU  WATAFTURU WOTE KWA PAMOJA NA BAADA YA KUFTURU NDIO KISOMO CHA KUMUOMBEA MAREHEM KITAANZA WOTE MNAKARIBISHWA.TAFADHALI UPATAPO TAARIFA HII MTAALIFU NA MWENGINE.

KWA WALE WASIOPAJUA NYUMBANI KWAKE KUNGSÄNGEN UNAWEZA KUMPIGIA UTAKAPOSHUKA KWENYE TRAIN AU BUS NA UKAPEWA MAELEKEZO KWA NAMBA 0762819664 COMVIQ




MUNGU ACHEZEWI JAMANI NINI WAJIFUNZE WAFUASI WENU?

 MAMBO yameiva, Jumamosi iliyopita serikali ilitimiza ahadi ya kuwaonesha wabunge mkanda wa video wa mtandao haramu wa biashara ya madawa ya kulevya, ulio chini ya viongozi wa dini nchini.

Kufuatia mkanda huo, Uwazi lina habari kamili jinsi kikosi  kazi cha  kupambana na  madawa ya kulevya chini ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,  Godfrey Nzowa, kilivyomnasa Askofu  Mkuu wa Kanisa la Lord Choose Charismatic Revived Church, Chidi Okechu.

 Okechu ambaye kanisa lake lipo Biafra, Kinondoni, Dar es Salaam ndiye anatajwa kuwa mkuu wa mtandao wa viongozi wa dini wauza madawa ya kulevya nchini.

ASKOFU NDEGE  TUNDUNI
Kwa mujibu wa Uchunguzi wa Uwazi, Machi 4, 2011 usiku wa manane, Kamanda Nzowa aliongoza kikosi chake na kuvamia nyumba aliyopanga askofu huyo, Kunduchi, Dar na kumkuta akiwa na kg 81 za heroine.

Askofu huyo alikamatwa akiwa na wapambe wake, Hycenth Stan, raia wa  Afrika Kusini, Shoaib Mohamed, Pakistan na Paul Ikechuwi Obi wa Nigeria, wote walikutwa kwenye nyumba hiyo yenye namba 593

KUNDUCHI NI PEPO YA WAUZA UNGA?
Uwazi limebaini kuwa mbali na askofu huyo na wapambe wake, msako mwingine wa Februari Pili, 2011, uliwezesha kunasa watuhumiwa wengine wa biashara ya madawa ya kulevya waliokutwa na kg 179, Kunduchi.

Waliokamatwa ni Fred William Chonde, mkazi  wa Mbezi Beach, Dar pamoja na raia wa Pakistan, Shahbaz Malik na Abdul Ghani ambao mbali na kukutwa na unga, pia walikutwa na shilingi milioni 15 kwenye gunia.
Habari zinasema, Februari 4, 2011, Abdallah Rajabu  alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar akiwa amemeza pipi 54 za cocaine, Juni Mosi, mwaka huu, Mwanaidi  Ramadhan Mfundo,  raia wa Kenya  na Watanzania Sara Daud Mnuo, Antony Athur Karanja  na Ben Nganer walikamatwa na kg 5 za cocaine na heroine.

Machi Pili, mwaka huu Chime Ajana alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar akiwa na kete 54 za cocaine, akijaribu kusafirisha kwenda Nigeria.
Habari zinasema kuwa watuhumiwa hao waliokamatwa ndiyo waliotoa siri nzito za viongozi wa dini wauza madawa ya kulevya, ikiwa ni pamoja na kuwezesha mtego uliomnasa Askofu Okechu.

MZEE WA KANISA NAYE MBARONI
Mzee wa kanisa moja ambalo halikutajwa, Raymond Gilbert Jungulu naye amekamatwa.

Wengine ambao wapo mahabusu wakituhumiwa kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya ni Bosi Chizenga, Ally Haji Mitanga, Gaban Abubakar na Gabar Diagar.

VIONGOZI WA DINI WAUZA UNGA NI WENGI
Kamanda Nzowa aliliambia Uwazi kuwa orodha ya wauza unga aliyopewa Rais Jakaya Kikwete  mwaka jana ipo na ina majina mengi ya viongozi wa dini.

Ripoti za kipolisi zinaliingiza matatani Kanisa Katoliki pamoja na Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata), kwa maelezo kuwa kuna wauza unga ambao wamekuwa wakitumia mwamvuli wa taasisi hizo za dini.


Habari zinasema kuwa baadhi ya watu wasio waaminifu, huingia mpaka kwenye msafara wa Papa Benedict XVI na kupitisha unga kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa kuwa hawakaguliwi.


PENGO AIUDHI SERIKALI
Hatua ya serikali kuliambia bunge kwamba Kanisa Katoliki nalo ni mwamvuli wa biashara hiyo haramu, imekuja baada ya Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kadinali Polycarp Pengo kuitibua ikulu.


Uchunguzi unaonesha, serikali ilichukizwa na kauli ya pengo kumwambia JK kwamba ni msaliti na hana ujasiri kama mwanamke mjamzito kwa sababu hajataja waziwazi majina ya watuhumiwa.


MAKANISA YA KIROHO YACHAFUKA
Gazeti hili limebaini kuwa tangu skendo ya viongozi wauza unga itajwe kwa mara ya kwanza na JK hivi karibuni, makanisa ya kiroho yamechafuka, huku viongozi wao wakituhumiwa moja kwa moja.

Pamoja na tuhuma hizo, Uwazi limebaini kuwa Askofu Zachary Kakobe, Mchungaji Getrude Rwakatare, Nabii Josephat Mwingira, Askofu Moses Kulola, Mchungaji Josephat Gwajima na wengineo ni wasafi, kwani bado hawajaingizwa kwenye skandali hiyo.

Baadhi ya maofisa  wa kikosi  kazi  waliongea  na mwandishi  wa habari  hii kwa sharti la kutotajwa majina yao walisema: “Nzowa yupo makini sana na kazi yake na angekuwa mtu mwenye tamaa ya fedha asingepata mafanikio.”

Nzowa alipozungumza na mwandishi wetu alisema: “Ninachoomba nipewe ushirikiano na wananchi kwa kuwa wao ndiyo askari wa kwanza.”

WABUNGE VILIO
Habari zinasema, baadhi ya wabunge walishindwa kuficha hisia zao na kutoa machozi walipokuwa wanaona mkanda wa video unaoonesha mtandao wa viongozi wauza unga.
Wabunge, walikwenda mbali zaidi na kushauri viongozi wote wa dini wauza unga wanyongwe.

Kwa hisani ya global publishers.

IMEKAAJE HII YA MASTAA WETU NA WAO NDIO VIO VYA JAMII!!!!