Saturday, March 24, 2012
HUDUMA DUNI YASABABISHA KIFO CHA MCHEZAJI INDIA
CHEZA soka nchini India amefariki dunia baada ya kuanguka na kuzirai wakati akicheza mpira ikiwa ni siku chache baada ya mchezaji wa Bolton Wanderers Fabrice Muamba kukumbwa na tatizo kama hilo katika mchezo wa Kombe la FA nchini Uingereza Jumamosi iliyopita. Mchezaji huyo anayeitwa D Venkatesh mwenye umri wa miaka 28 alianguka baada ya moyo wake kusimama kufanya kazi ikiwa ni muda mfupi baada ya kuingia uwanjani kama mchezaji wa akiba wakati wa mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza kati ya timu yake ya Bangalore Mars dhidi ya South Western Railway. Vyombo vya habari nchini humo vimesema kuwa hakukuwa na na gari la wagonjwa uwanjani hapo wakati tukio hilo lilikitokea hivyo kupelekea mchezaji huyo kukimbizwa hospitali na pikipiki za miguu mitatu maarufu kama Bajaj. Taarifa hiyo pia ilithibitishwa na Shrikisho la Soka nchini India-AIFF juu ya kifo cha mchezaji huyo ambaye alifariki wakati akifikishwa hospitalini.
Thursday, March 22, 2012
BINADAM MWENZETU HUYU ANAOMBA MSAADA WETU JAMANI
MTOTO Honolata Juma Christian (8), (pichani) mkazi wa Mgeta wilayani Mvomero aliyetelekezwa na ndugu zake kutokana na maradhi ya ajabu yanayo msumbua, anataabika katika hospitali ya rufaa mjini hapa akiomba msaada wa shilingi 1,000,000 ili akatibiwe.
Gharama hizo ni za tiba,usafiri na matumizi katika Hospitali ya KCMC ya mjini Moshi ambako ameshauriwa kwenda na madaktari wa hospitali ya Mkoa wa Morogoro alikolazwa.
Honolata ambaye tangu kuzaliwa kwake amekuwa akisumbuliwa na magonjwa likiwemo la kuota nywele mwili mzima, nundu mbili kichwani mithili ya pembe na matatizo ya macho.
Mtoto huyo analelewa na mama yake mzazi, Grace Francis (30) ambaye anadai ndugu zake wamemsusia na hawataki kumsaidia.
Akiwa hospitalini hapo wodi namba nne , Uwazi lilizungumza na mama huyo ambaye alisema mtoto wake hivi sasa ameshindwa kuendelea na masomo kutokana na maradhi hayo ya ajabu.
“Amefanyiwa uchunguzi na kugundulika kuwa jicho moja limekufa na asipopata tiba mapema la pili nalo litakufa, naomba msaada kwenu wasamaria,” alisema mama huyo huku akitokwa na machozi.
Akaongeza: “ Baada ya baba yake , Juma kufariki kwa kugongwa na gari shemeji,wifi na wakwe zangu wakamkataa wakisema sisi hatumtambui huyu mtoto mwache afe…nikaanza kuhangaika mahospitalini ikiwemo CCBRT ambako walimfanyia oparesheni ya jicho la kushoto ambalo anatumia kuonea,” alifafanua Grace.
Walioguswa na habari hii wanaweza kumsaidia kwa kuwasiliana naye kwa namba ya simu 0713778024.

Wednesday, March 21, 2012
NYUMBA YA SPIKA WA BUNGE IMEGHARIMU TSH BILION 1,5
Hatimaye Spika wa Bunge la Tanzania pale Dodoma atakuwa na makazi rasmi baada ya ujenzi wa nyumba ya Spika kukamilika na makabidhiano kufanyika. Nyumba hiyo ambayo ipo maeneo ya Uzunguni nje kidogo ya Dodoma mjini imegharimu takribani Tshs 1.5 Billion na imejengwa na kampuni ya Pacha Building Construction Company. Hii inakuwa nyumba ya kwanza rasmi ya Spika kwani hapo awali hapakuwahi kuwa na nyumba rasmi ya Spika
MABADILIKO YA MUDA WA SIKU YA KISOMO CHA MAMA YAKE USTADH MAN NA KARAMA
USTADH MAN NA MDOGO WAKE KARAMA WANAPENDA KUWATAALIFU NDUGU NA JAMAA WOTE WA STOCKHOLM NA NJE YA STOCKHOLM KWAMBA WATAFANYA KISOMO CHA MAMA YAO MZAZI ALIOFARIKI NYUMBANI TZ SIKU YA JUMAPILI NA KUZIKWA JUMATATU.
KISOMO KITAFANYIKA VISBYRINGEN 6 RINKEBY SIKU YA JUMAMOSI YA TAREHE 24-03-2012 SAA SABA (13:00PM)MCHANA WOTE MNAOMBWA KUFIKA KWANI KUFIKA KWENU NDIO KUFANIKISHA KISOMO HICHO.TAFADHALI MJULISHE MWENGINE UPATAPO TAARIFA HII ASANTENI.

Subscribe to:
Posts (Atom)