Huyu ni rafiki yangu toka kitambo sana kabla yeye ajawa Rado na mimi sijawa Kc.Kwapamoja tumekaa chini na kujipanga katika mikakati ya life ya bongo na nje ya bongo na kwa upande wa bongo tumeanza na duka la nguo.Watu wetu tegemeeni vitu vingi vitakuja ndani ya temekepamoja si tu biashara ya nguo kuna biashara nyingi zitakazoletwa na temekepamoja.Kwanini tumeamua kua temekepamoja na si darstockholm?Tumefikia makubaliano haya baada ya kuona tunahitaji temeke yetu tujivunie nayo na ndio maana sote kwa pamoja tukaafikiana kutumia Temekepamoja kama kampuni yetu na tumeanza na duka la nguo.Ningependa kuwajulisha wadau wangu wooote wa darstockholm.blogspot.com sitopost kitu chochote kwenye darstockholm.blogspot.com kuanzia leo fungua www.temekepamoja.blogspot.com humu utapata picha na matukio ya sweden,bongo na nchi zingine zote kama kawaida kama unataarifa,tangazo,tukio na picha au habari yoyote tutumie kwenye temekepamoja,ingia utapata email na namba za simu.Nawaomba radhi kwa usumbufu nitakaowasababishia.
Mwanzo mgumu duka letu tulianza hatua za mwanzo kama hvi.Hapo tukiweka tires
tukavunja ukuta na kuweka geti kama unavyoona mdau wetu.
Mtazamo wa nje ukilifungua geti wakati ujenzi unaendelea.
Hapa imeanza kupatikana taswira ya mlango wa duka na hatua za mwisho.
Mtazamo kwa nje baada ya robo tatu ya ujenzi kukamilika.
Kwa ndani mabadiliko yameshaonekana.
Hapa sasa tayari temeke pamoja classic wear ikazaliwa rasmi.
Mtazamo wa ndani baada ya kuweka nguo zakutoka china,thailand na turkey mchanganyiko.
Ukiwa ndani mteja utavuta pumzi vizuri kwa kiyoyozi a.k.a kipupwe huku unachagua nguo.
Hapa utapata jezi pia za team za uingereza kama Manchester,Arsenal,Chelsea,Liverpool na Manchester city.Tupo katika michakato pia na jezi za Newcastle ili mjomba Jj nae aje kutuunga mkono akiwa mapumziko Bongo.
Kwa wale wapenzi wa team za bongo kubwa kama Simba,Yanga na Azam tunazo jezi za rangi zote.Tunashukuru kwa hili swala la jezi za team za bongo tuliomba kibali kwa team husika na tumeruhusiwa kuuza rakini kwa kununua kutoka kwao wahusika na si uchochoroni karibuni.
Watu wangu wooote wa pande za Stockholm,Gothenburg,Uppsala.Watu wangu wa Holland,England,South Africa,Germany,Belgium,Italy na kwengineko,kwa wale woote wanaotokea temeke na hata kama sio temeke kama unamfaham Kc na Rado mnakaribishwa sana utakapokua kwenye mapumziko yenu bongo mje mjipatie bidhaa temekepamojaclassic wear.
Azam kama kawa tumepata kibali kutoka kwao kuuza jezi zao dukani kwetu kama wewe shabiki wa azam karibu temekepamoja classic wear.
Kwa upande wa snikers,makobazi na kofia vyote vinapatikana hapo karibuni sana .
Kwa wale wa spray na nguo za ndani(boxer)zipo pia ukiingia utakutana nazo sample kwenye kabati hapo.
Soon mzigo mwingine utaingia kutoka china,thailand na turkey.Pia muda si mrefu wateja wetu watakaokuja kununua bidhaa temekepamoja classic wear watawekewa bidhaa zao kwenye mifuko yenye nembo ya temeke pamoja classic wear ndio tupo katika mchakato wa mwisho wakutengeneza nembo kweye mifuko.
Wooote mkaribishwa temekepamoja classic wear tunapatikana karibu kabisa na kona ya temeke sudan kama unakwenda temeke mwisho mtaa wa kwanza kushoto kwako,mtaa mkumbakaribu kabisa na balabala kubwa ya madaladala.Kwa maelezo zaidi utakua unapata kupitia www.temekepamoja.blogspot.com tutembelee kwenye blog yetu.
Ewe mwenyezi mungu tujaalie kheri kwenye utafutaji wetu kwa baraka zako amen.