Saturday, December 31, 2011

TANGAZO KWA WADAU WOTE.

WADAU WANGU NIMEPEWA TAARIFA NA KAKA MMOJA(JINA)YEYE AMENITUMA NIWATAALIFU ANA BIASHARA YA NONDO ZAKE KWA MDADA AU KWA MWANAUME YEYOTE ANAETAKA KWA AJILI YA NDUGU YAKE WA KIKE.KWA MAELEZO ZAIDI UNAWEZA KUWASILIANA NAE YEYE MWENYEWE KWA NAMBA   0738529448 YEYE ATAKUPA MAELEZO YOTE JUU YA JAMBO HILI.

NATUMAINI UJUMBE MTAKUA MMEUELEWA VIZURI WADAU WANGU NINAPOSEMA MINONDO.

Thursday, December 29, 2011

WAANDISHI RAIA WA SWEDEN WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 11 NCHINI ETHIOPIA

Mahakama nchini Ethiopia leo hii imewahukumu waandishi wa habari wawili wa Kisweden kifungo cha miaka 11 gerezani kutokana na tuhuma za kusaidia vitendo vya kigaidi na kuingia nchini humo kinyume cha sheria. 

Hukumu hiyo imetolewa baada ya kukoselewa na makundi ya haki za binadamu. Jaji Shemsu Sirgaga aliiambia mahakama hiyo kwa lugha ya Amharic kwamba adahbu yao ni kutumikia kifungo cha miaka 11 jela.
Mwandishi Martin Schibbye na mpiga picha Johan Persson walikamatwa huko katika mkoa wa Ogaden Julai mosi, wakiongozana na waasi wa wa eneo hilo wa chama cha Ukombozi wa Ogaden, ONLF, baada ya kuingia Ethiopia kutokea Somalia. 

Kufuatia hatua hiyo ya kuwatia hatiani waandishi hao wa habari, waziri mkuu wa Sweden, Fredrik Reinfeldt, amesema watuhumiwa hawana hatia na kutaka waachiwe huru. 

Waasi wa ONLF wamekuwa wakipigania uhuru wao huko katika mkoa wa Ogaden kutoka kwa serikali ya Ethiopia tangu 1984, wakidai kwamba wanatengwa na utawala wa nchi hiyo.

MSICHANA WA MIAKA 9 AFARIKI BAADA YA KUTAHIRIWA


Ngariba wa miaka 70, mkazi wa kijiji cha Irienyi Kinesi, wilayani Rorya, mkoa wa Mara, Nyaisanga Marwa, amekamatwa na Polisi na anatarajia kufikishwa mahakamni kujibu mashitaka ya kumkeketa mwanafunzi wa darasa la pili wa Shule ya Msingi Irienyi (jina tunalihifadhi) na kumsababishia kifo, baada ya kutokwa na damu nyingi kwenye sehemu aliyokatwa.

Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Tarime/Rorya, Justus Kamugisha, jana alisema kuwa, tukio hilo lilitokea Desemba 19, mwaka huu, katika kijiji cha Irienyi Kinesi, wilaya ya Rorya na kwamba baada ya mtoto huyo kukeketwa, alitokwa damu nyingi iliyoendelea kutoka bila msaada wowote kwa matumaini kuwa atapona kwa miti shamba.

Kamanda huyo alisema, Desemba 23, mwaka huu, mtoto huyo (9) alipoteza maisha na kwamba Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na ndugu wa marehemu walimkamata ngariba huyo kabla hajatoroka na hadi sasa yupo mikononi mwa Polisi na wanatarajia kumfikisha mahakamani wakati wowote kujibu shitaka la kukeketa na kusababisha kifo.

Tuesday, December 27, 2011

TANGAZO KWA WADAU WOTE WA DARSTOCKHOLM

KAMA WEWE NI MMOJA WA WATU WANAOTUMIA MUDA WAO KUTAZAMA BLOG HII TANGAZO HILI LINAKUHUSU.KATIKA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA WA 2012 NIMEONELEA TUSHEREKEE KWA PAMOJA KWA STYLE HII,NAJUA KILA MTU ANAJUA WAPI ATAUSUBILIA MWAKA MPYA KWA HAMU KUBWA KUSHANGILIA KWA KUUFIKIA AKIWA HAI NA MWENYE AFYA TELE,SASA BASI KWA PAMOJA NINGEPENDA TUWEKE PICHA ZETU ZA MATUKIO YA KUKARIBISHA MWAKA 2012 KATIKA BLOG YETU YA DARSTOCKHOLM.

SASA KWA YEYOTE AMBAE ATAKUA TAYARI KUTUNDIKA PICHA YAKE AKISHEREKEA MWAKA MPYA.NAOMBA NIELEWEKE VIZURI WADAU WANGU UKIWA WEWE UNATUMIA MUDA WAKO KUTAZAMA BLOG HII  UNAWEZA KUNITUMIA PICHA YAKO NA NITAIWEKA BILA KUJALI CHOCHOTE,NITUMIE KWA EMAIL IFUATAYO.
                                       kessbr@yahoo.co.uk
                  ASANTENI.

ALBUM YANGU YA LEO HII HAPA




























Friday, December 23, 2011

SAIDI MBEGU AMVISHA PETE MCHUMBA WAKE PICHA ZINASEMA

                                         Kupiga goti ndio sharti ya tukio kama hili












                                        Furaha ilitawala siku hyo kwa wapendanao hawa.






                                               Tingisha tusheherekee kwa pamoja

Kiukweli hatua waliofikia wapendanao ni kubwa sana na kwa upande wangu nawapa ongera na kuwaombea dua ili wafikie lengo katika maisha yao amen.

Wednesday, December 21, 2011

MVUA YALETA MAAFA MAKUBWA JIJINI DAR



                                    _Huwezi amini hii ndio dar kwa sasa
                                  Balabala ya morogoro eneo la jangwani
                                  Wananchi wakitembea kwa miguu,usafiri hakuna jijini
                                   Hili ni daraja la salender limekumbwa na mafuliko
     
         Wananchi wakijaribu kuokoa maisha yao kutokana na makazi yako kujaa maji yaliotokana na mvua kubwa zinazoendelea jijini dar..Asante michuziblog.