Tuesday, June 26, 2012

WADAU WANGU NIMEATHIRIKA NA HUU UGONJWA WA HIVI VITU NAOMBENI DAWA PLZZ AU HATA USHAURIKWELI MWISHO WA UBAYA NI ....

MSIBANI KUNAPOCHAFUKA NA MAPANGA SHAAA

 Stori nzima ilikua hivi.Nina rafiki yangu wa karibu alifiwa na baba yake mzazi,alinipa taarifa ili nihudhulie mazishi,nilisimamisha pilika zangu na kutokea msibani tayari kwa mazishi nilipofika nilikutana na haya..
 Marehem alikua muislam na akawahi kubadili dini na kua mkristo baada ya kupendana na mwanamke mkristo na akazaa nae mtoto wakiume ambae nae alikua mkristo ila mtoto wake huyo huyo baadae alibadili  dini na kua muislam.Ilipita mwaka mtoto wa marehem alibadili tena na kurudi katika ukristo na mpaka sasa yupo katika imani ya ukristo.
Haikujulikana kama mzunguko huu wa kubadili dini ungeweza kuleta tabu baadae,sasa ikawa kivumbi baba mzazi wa huyu kijana alipofariki kwani mtoto anataka baba yake azikwe kikristo na ndugu wa marehem ambao wote wakristo wanataka ndugu yao azikwe kislam yakaanza malumbano.......
Baada ya muda nikiwa nimejisahau kushika camera walitokea watu kama kumi wakiwa na mapanga na kuanza kuwapiga watu na mabapa ya upanga na wengine kukata tulubai na miti ya tulubai,kiukweli zikaanza mbio za mita mia ila alikosekana usein bolt tu na pia refa hakuwepo.....
mimi pia sikua nyuma katika wakimbiaji ila chakushangaza nilisahau kuibeba gari maana hata magari yalipigwa mapanga.Baada ya muda kukatulia ndio vikaanza vifungu vifungu kujadili lakini wenye mapanga walikaa pembeni na kusema hatutaki msiba ondokeni na jeneza likija hapa tutalivunja.Mpaka naondoka eneo latukio msiba ukavunjwa katika hyo nyumba na mtoto wa marehem akaambiwa atafute nyumba atakayoweka msiba na sio pale nyumba ya waislam aweke msalaba.Dah duniani kuna vituko sana,kesho nitawasiliana na mtoto wa marehem nakujua msiba ulikwenda vipi na walizikaje au bdo marehem hajazikwa?nitawajuza wadau

Friday, June 22, 2012

SHEREHE ZAKUMALIZA SHULE ADAM KASSA

       Adam Kassa akiwa katika nyuso ya furaha ongera kaka kwa kuhitimu
     Mjeru miongoni mwa walioudhulia shughuli hyo akiwa ndani ya jumba matata
      Wazazi wa Adam Kassa      Uondo wa ngoma uingie ucheze na hasa ukicheza na mwenza wako Chalz na mkewe
      Ilikua wawili wawili hapa Mjeru na shemeji yangu wa ukweli
     Hapa mama Hakeem,Aida a.k.a mtarajiwa pale Damu yangu baba Hakeem nice pic

      Linda na Lilian marafiki wa ukweli nao walikuwepo kwenye mnuso huo
   Mtamboni dj Richie


      Cheda boy akiwa na Adam Kassa

Thursday, June 21, 2012

FC KILIMANJARO YAFANYA MAUAJI KWA TIMU YA CHILE 13 KWA 2

            Kikosi kamili cha fc kilimanjaro wakiwa na mlezi kaka Liban
     Capten mstahafu Jj akiwa na Capten mpya Abui

     Capten Abui Fuad na mfumania nyavu hatari wa Fc Kilimanjaro Abuu Mkangwa  a.k.a mvuvi
    Edger Davids miwani hyo kwani mwisho wa kuivaa ujaisha!
     Hapa Fc Kilimanjaro wakiwa mapumziko tayari kwa kupata mawaidha.
      Meneja Nyupi
     Naona benchi la ufundi liliongozwa mchezaji wa kimataifa Machupa
      Baada ya kushusha kipigo kinachofata ni kuwapa pole
                          Majembe ya Fc Kilimanjaro

Wednesday, June 20, 2012

KARIBU BONGO HOME BOY CHALZ A.K.A GABU

 Haya Jembe ardhi ya bongo ndio umeshatimba michakato ndio ile ile karibu sana mkubwa.

 Ndugu pia walijitokeza kumlaki ndugu yao walioachana muda mrefu,wote wakiwa na furaha
     
Akiwa ndani ya kimeo cha darstockholm tayari kwa kumpeleka uswazi akapumzike karibu mwana

IPO KWA FUNDI

Wadau wangu tuvumiliane kidogo kwa ukimya blog yetu ipo kwa fundi kidogo kwa ajili yakuiboresha zaidi,muda c mrefu nitawarushie nitakavyovikamata.Ila nitakua nadokoa dokoa huku tukimwachia fundi akifanya kazi yake.

Na wale wadau wangu wenye tukio nitumie kwa email binkaramabr@Yahoo.com nitalitundika bila kujali hunipendi au sikupendi tofauti zetu nje ya blog hii ni yetu wote.

Sunday, June 17, 2012

TAARIFA YA KISOMO

NDUGU ISMAIL MAARUFU BIG ALIEFIWA NA BABA YAKE MZAZI HIVI KARIBUNI,ANAWATANGAZIA KISOMO CHA MZAZI WAKE HUYO.

KISOMO KITAFANYIKA TAREHE 23/06/2012  MAHALI VALUNDA VAGEN 31,UPPLANDS VASBY.MUDA NI 16.00PM SAA KUMI JIONI.

TUNAOMBWA KUZINGATIA MUDA,UPATAPO TAARIFA HII MJULISHE NA MWENZIO KWANI KUFIKA KWAKO NDIO KUFANIKISHA KISOMO CHA BABA YETU MPENDWA.

KWA MAELEZO ZAIDI UNAWEZA KUPIGA SIMU 0734790396,0761553869

WOTE MNAKARIBISHWA.

Wednesday, June 13, 2012

MAOJIANO JUU YA MAISHA NA VIJANA WENYE NDOTO ZAKUFIKA ULAYA NDANI YA TIMES FM

                                 umakini unahitajika kiukweli kuzungumza kwenye media
                                 Mshkaji mkali sana katika mix alinivuta nichungulie
                                 Jabir big jah akiteta jamb na dj wake


     Niliongozana na swahiba Rama Rado a.k.a kichomi mpitie ktk temekepamoja.blogspot.com
                     Nikipewa maelekezo juu ya mitambo na ufanyaji wake kazi
     Ikafika muda wa kushow love hapa dada wa kipindi cha mapenzi kinachoanza kila sa nne ya bongo
Wadau wangu kiukweli si kazi ndogo kuzungumza katika media ambayo watu dunia nzima wanakusikia,nilijitahidi kadri ya uwezo wangu nadhani kwa wale mlionisikiliza mmesikia the way nimeongea.Sema ilikua hatari pale nilipoambiwa nitoe ushauri juu ya vijana wenye ndoto zakwenda ulaya nilitamani niseme wasije lakini je wangenielewa pale wangeniona mm nilivyo kwa sasa.Niliwashauri wajipange na maisha popote ila siri ya jandoni apewi asieingia jandoni na huondo wa ngoma ingia ucheze.