Monday, April 30, 2012

DIAMOND MSANII WA KWANZA KUTUMIA HELKOPTA KUINGIA KWENYE SHOO NDANI YA DAR LIVE

                                  Diamond akielekea kupanda Helkopta

                                                     Saluuuuuuuuuute
                                 Diamond akiomba mungu kabla ya Helkopta kuondoka
                                 Ukumbi wa Dar live ukionekana kwa juu
                                 Sasa Diamond akitua ndani ya mbagala
                                 Mashabiki wakimsindikiza Diamond kelekea ukumbini
                                 Diamond akishuka ktk gari tayari kuingia ukumbini
                                 Umati wa watu waliokua wanamsubiri Diamond

                                 Diamond akiwapungia mkono mashabiki waliompokea
                                 Mashabiki walipagawa baada ya diamond kutua

Friday, April 27, 2012

TANGAZO LA UFUNGUZI WA CHAMA CHA WATANZANIA SWEDEN

                                         CHAMA CHA WATANZANIA SWEDEN
Kwa Watanzania pamoja na marafiki!

Kamati ya muda ilioteuliwa Ubalozini kwa nia ya kuanzia chama cha watanzania Sweden,inawakaribisha katika hafla fupi ya ufunguzi wa chama na pia kuchagua viongozi watakaoendeleza shughuli za chama.

Mgeni wa heshima katika ufunguzi na uchaguzi wa viongozi wa chama cha watanzania atakua
              Mh.balozi  Muhammed Mwinyi Haji Mzale.
Sehemu:Tanzania House,Näsby Alle 6,Täby

Wakati:Saa tisa mchana mpaka saa kumi na moja  jioni terehe 28-04-2012 jumamosi.


Mwaliko utatumwa kwa barua pepe ikiambatanisha fomu za kujiandikisha kugombea uongozi wa chama.Pia waweza kupakua katika tangazo lilowekwa katika mtandao wa Ubalozi.

           Wote mnakaribishwa  na ukipata taarifa hii tafadhali mtumie na mwingine!
                           
                             Kamati ya wanamchakato kupitia
                                         Katibu wa muda


                                      Bi. Angela Wilberd:
                                tanzanianswe@hotmail.com

SUMA LEE-UTANIKUMBUKA


HII HAPA HELKOPTA ATAKAYOSHUKA NAYO DIAMOND NDANI YA DAR LIVE MBAGALA

Msanii aliejuu kwa sasa ndani ya bongo Diamond akipata picha katika helkopta atakayotumia kwenda nayo kwenye show yake ndani ya Dar live iliopo mbagala.Upo juu jembe.

TIPTOP CONNECTION-KIBOKO YAO


DAH HIKI KILIO CHA LULU KINAELEZA JAMBO SEMA HAKUNA ANAEMSIKILIZA

Kiukweli kabisa ukimtazama hapa Lulu utajua kabisa ndani ya moyo wake si bule analo anachokililia kwa uchungu ila hakuna wakumsikiliza,Maana mtendaji husika wa jambo tena wa mauaji kufikia hatua ya kutoa chozi la hisia kama hili ni hadimu sana.Ila usijali mdogo wangu mungu siku zote anasimama na kwenye haki ya mtu Inshallah kwako atasimama na tutagongana kitaa kama kawa,pia tunawaomba wahusika haki isimame vizuri bila kuongezeka lolote ili huyu mtoto aipate haki yake.

OFFSIDE TRICK-AAMBIWE BABU JINGA


MADEE-HISTORY


REY ATOA DUKUDUKU LAKE BAADA YA KUENEA HABARI AMEHUSIKA NA KIFO CHA KANUMBA


Yapata wiki tatu sasa tangu msanii mwenzangu Steven Kanumba aage dunia, na kama ilivyo kwa kila kitu kinapotokea huandamana na kila aina ya maneno na hisia mbali mbali kutokana na mitazamo ya watu kupishana kuhusiana na jambo husika. Kulingana na muktadha huo, msiba wa Steven Kanumba umekumbwa na maneno na hisia kama hizo, hususan mazingira ya kifo chake; kinachosikitisha zaidi watu wengi (ambao wanajitambulisha kama wapenzi wa Kanumba), na baadhi ya vyombo binafsi vya habari vimekuwa vikinihusisha na kifo hicho, kwa kusema kwamba kwa njia moja au nyingine ninahusika na mauaji ya Steven Kanumba. Kwa muda wote huo tangu msiba ulipotokea mpaka leo hii nashika kalamu kujaribu kuyaweka sawa na kuondosha hisia chafu katika fikra za watu, nimekuwa nikipitia katika wakati mgumu sana kwa jinsi ambavyo nimekuwa nikinyooshewa vidole kila upande nikihusishwa na kifo hicho, kiujumla nimezingatia maoni ya wapenzi ya mashabiki wangu wakinitaka kuwa na subira,  ila kuna ukweli usemao kwamba, uongo ukirudiwa sana jamii huusadiki na kuuona ukweli, nimeona nisikae kimya ila niweke sawa hili kwamba sihusiki na kifo cha Steven Kanumba.
Nasema wazi kwanza sihusiki kabisa na kifo cha Kanumba kwanza kwa kuzingatia mazingira yenyewe ya kifo kilivyotokea. Wakati kifo hicho kinatokea, nilikuwa sehemu nyingine kabisa na mimi nilikuwa mtu wa tatu kutaarifiwa kwamba Kanumba amepatwa na mkasa ambao baadae ulisababisha kifo chake. Na na hata nilipofika katika hospitali ya Muhimbili (tofauti na watu wanavyodhani kuwa nilifika nyumbani kwake; ukweli mimi nilimkuta tayari amepelekwa Muhimbili), nilikuta tayari alikuwa ameshafariki ndio maana hata Polisi wanaohusika na usalama wa raia, si tu kwamba hawakuniweka chini ya ulinzi, sikuitwa hata kuhojiwa kwa sababu hakuna mazingira yoyote yanayonihusisha mimi na kifo hicho.
Pili, watu wanahusisha tofauti za kibinadamu zilizokuwepo baina yetu na kifo hicho, nasema hii sio sahihi kwa sababu kwanza ni kawaida kwa binadamu kutofautiana, isipokuwa kwetu sisi baadhi ya vyombo vya habari vilikuwa vinakuza kwa sababu nisizozijua, hivyo jamii ikachukulia kuwa tofauti zile ni uadui kitu ambacho sio sahihi, kwani sisi hatukuwa watu pekee tunaotofautiana kwani huu ni mwenendo wa kawaida wa dunia; hivi jana tumeshuhudia Waziri mmoja akieleza bayana katika mkutano na waandishi wa habari kuwa na tofauti na naibu wake, lakini hatuajasikia ikiandikwa wana ‘bifu’ bali imetafutwa lugha nzuri ya kupamba tofauti hizo, kwa kuwa waliohusika ni waheshimiwa, ila kwa wengine kutokana na sababu tusizozijua, inaonekana kama ni haki yetu kuandikwa vibaya. Kinachosikitisha, kwa nini jambo hili linachukuliwa kwa mkazo mkubwa sana, kwani hatujawahi kusikia watu wakiwa wanatofautiana na ndugu jamaa hata na marafiki zao na inaonekana kawaida tu? Kwani vyombo vya habari havikuwahi kuandika kuwa marehemu Steven Kanumba alikuwa na tofauti na baba yake, na yeye mwenyewe alitamka hivyo katika vyombo vya habari, mbona wameliongea bila kuongeza chumvi, na jamii inaona kuwa ni jambo la kawaida la kibinadamu.
Pengine watu wanaojaribu kuongea hayo, hawajui mimi na Steven Kanumba tumetoka wapi? Sisi si watu tuliokutana barabarani, tuna historia katika kazi yetu ya sanaa na pia katika maisha maisha yetu. Mwanzoni kabisa, mimi ndiye niliyempokea Kanumba pale Kaole na ndiye niliyemfundisha sanaa pale (nadhani watu wanakumbuka tamthiliya za wakati huo ITV) na baada ya hapo tulienda pamoja katika kampuni ya Game 1st Quality pamoja na tukafanya filamu kama Johari, Sikitiko Langu, Dangerous Disire na nyinginezo, na tuliendelea kuwa pamoja katika kampuni hiyo mpaka tulipofanya filamu ya Oprah mwaka 2008 ambapo niliingia rasmi kufanya kazi za kampuni yangu, lakini tuliendelea kuwa pamoja hata wakati nikiendelea na kazi za kampuni yangu. Pia mimi nilikuwa wa kwanza kuanza kufanya kazi na Steps na baadae Kanumba alipoanza kufanya kazi zake mwenyewe na kunikuta huko tuliendelea kuwa pamoja kama siku zote. Kitu kikubwa kilichokuwa kinaendelea baina yetu, ni kwamba tulijenga ushindani wa kuendeleza kazi mbele kwa kila mmoja akitoa kazi, mwingine anamjibu,  Isitoshe hata vitu vyetu binafsi utaona kama kuna kufanana; kuna wakati Kanumba alinunua Toyota Ruv 4 nyeusi mimi nikanunua ya kijani, aliponunua Harrier na mimi nikanunua pia, na hata gari za hivi karibuni, ukitazama utaona kuwa zinafana kwa karibu; hii ilikuwa ni kama maisha yetu, hatukuwa na uadui, ilikuwa tunapeana changamoto za maendeleo.
 Watu wanaojaribu kuonesha kuwa tofauti zetu ilikuwa ni uadui, huwa hawajui wapi tulikotoka ndio maana wanasema wasemavyo na katika kuthibitisha kuwa tofauti hizo hazikufikia katika uadui, kuna watu ambao wanafanya kazi nami katika kampuni yangu ya RJ ndio hao hao Kanumba alikuwa anawatumia siku zote katika kazi zake, hata baada ya tofauti hizo hakuna aliyekoma kufanya kazi na yeyote kati yetu. Hii inathibitisha kuwa tofauti ilikuwa kati yetu kama binadamu, sio chuki za kimafanikio, ingekuwa hivyo watu kama Junior Syaary ambaye mara nyingi hufanya final editing katika RJ ndio huyo huyo alikuwa akifanya na Kanumba, Ally Yakuti ambaye anaandika script za RJ, ndiye huyo huyo aliyekuwa anaandika kwa Kanumba, Steven Shoo ambaye ni mtaalamu wangu wa light, ndiye huyo huyo anayetumiwa na Kanumba na wengine wengi kama Juma Chikoka aliyecheza kikamilifu katika filamu ya kijiji cha Tambua Haki, ambaye pia anashiriki filamu nyingi za RJ, na wote hao, hawakuanzia kwa Kanumba, wote wameanza kwangu mimi ndio niliompatia na hata baada ya hayo yanayosemwa kuwa kuwa ni uadui, sikuwahi kuwakataza kufanya kazi na Kanumba.
Tatu kumtuhumu mtu kwa namna yoyote ile bila ya uthibitisho wa tuhuma hizo, ni kosa kwa sheria za nchi na pia kama ni mfuasi wa dini yoyote ni dhambi, kwani wakati ukisema hayo huku hujui uhalisia bali unasukumwa na nguvu za hisia tu ni sawa na kumchafua mtu huyo katika jamii bila ya kujua jamii inamchukuliaje. Napenda kusema wazi wazi kuwa, kwa kila anayetekwa na wimbi hili, ajaribu kufikiria leo ipo kwangu mimi, kesho inaweza kuhamia kwako, kwani mimi sio wa kwanza kufikwa na haya, inaweza kukukuta hata wewe au ndugu yako, utajisikiaje. Na kama kweli mimi nimehusika na kifo cha Kanumba kwa namna yoyote ile, basi Mungu atanihukumu na kila aliye hai atashuhudia, ila kama sijahusika kwa lolote, Mungu hatonihukumu na badala yake ataniinua, kwa kuwa ninapita katika kipindi kigumu mno sasa hivi kwa madhila haya.
Mwisho kabisa napenda kumaliza kwa msemo usemao, ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke, kwani kadri mambo haya yanavyoendelea, usidhani yataishia kwangu, kwani mkono wa dhuluma haushii karibu, ukisikia jirani anapiga kelele za mwizi, usilale kamsaidie, usiseme kuwa hatuhusiki kwani hayupo kwetu, kesho utafikwa na wewe utakosa wa kukusaidia. cha msingi kama tunampenda sana ndugu yetu ni kumuombea kwa Mungu, kwani hatujui makao yake huko aliko, na sio kuunda vitu ambavyo kamwe hata yeye angekuwa hai asingeviafiki.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA MAHALI PEMA PEPONI
MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA 
Source: ray the greatest blog

Monday, April 23, 2012

KESI YA LULU YASOGEZWA TENA MPAKA MEI 7 ARUDISHWA RUMANDE

 Msanii Elizabert Michael mwenye dira jekundu (LULU)akiwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la magereza,tayari kuelekea kutajwa kesi yake inayomkabili ya mauaji ya msanii Steven Kanumba.
                                Chini ya ulinzi mkali sana mtuhumiwa Lulu
Mtuhumiwa alipandishwa mahakani kwa kutajwa kwa kesi yake hiyo ambayo upelelezi wake haujakamilika.Kesi hyo itasomwa tena mei 7

Wednesday, April 18, 2012

TUKIFANYA SISI MZOZO USIO NA KIPOZO

Kwa hisani ya mjengwablog.

KWA WALE WATEMAJI YAI TUJUZENI HARAKA(Minister in 'racist circumcision outrage')

"In our view, this simply adds to the mockery of racism in Sweden," Kitimbwa Sabuni, spokesperson for the National Afro-Swedish Association (Afrosvenskarnas riksförbund) told The Local.

"This was a racist spectacle."

Sabuni's comments come following Adelsohn Liljeroth's participation in an art installation that took place at Stockholm's Moderna Museet in connection with World Art Day on April 15th.

As part of the installation, which was reportedly meant to highlight the issue of female circumcision, the culture minister began cutting a large cake shaped like a black woman, symbolically starting at the clitoris.

Makode Aj Linde, the artist who created the installation and whose head is part of the cake cut by the minister, wrote about the "genital mutilation cake" on his Facebook page.

"Before cutting me up she whispered, 'Your life will be better after this' in my ear," he wrote in a caption next to the partially eaten cake.But images of the event, which show a smiling and laughing Adelsohn Liljeroth slicing up the cake, have caused the National Afro-Swedish Association and its members to see red and issue calls for her resignation.

"According to the Moderna Museet, the 'cake party' was meant to problematize female circumcision but how that is accomplished through a cake representing a racist caricature of a black woman complete with 'black face' is unclear," Sabuni said in a statement.

According to Sabuni, the mere fact that the minister particiapted in the event, which he argued was also marked by "cannibalistic" overtones, betrays her "incompetence and lack of judgement".

"Her participation, as she laughs, drinks, and eats cake, merely adds to the insult against people who suffer from racist taunts and against women affected by circumcision," he said.

"We have no confidence in her any longer."

Speaking with the TT news agency, Adelsohn Liljeroth was sympathetic to the association's reaction, but nevertheless defended her actions.

"I understand quite well that this is provocative and that it was a rather bizarre situation," she said.

"I was invited to speak at World Art Day about art's freedom and the right to provoke. And then they wanted me to cut the cake."

However, Adelsohn Liljeroth said the National Afro-Swedish Association's anger should be directed at the artist, not at her, claiming the situation was "misinterpreted".

"He claims that it challenges a romanticized and exoticized view from the west about something that is really about violence and racism," she said.

"Art needs to be provocative."

But the minster's defence of her actions rang hollow for Sabuni.

"It's extremely insulting for the minister to claim that we've somehow 'misunderstood' racism," he said.

According to Sabuni, the incident is "strange" but "not unexpected" in the Swedish context.

"Sweden thinks of itself as a place where racism is not a problem," he said.

"That just provides cover for not discussing the issue which leads to incidents like this."

While a museum is certainly allowed to do what it wants as long as the laws are followed, Sabuni argued that a minister needs to be held to "higher standards".

"To participate in a racist manifestation masquerading as art is totally over the line and can only be interpreted as the culture minister supporting the Moderna Museet's racist prank," he said.

RECHO-UPEPO

BARNABA-GUBEGUBE

AT-UNATAMANI

Tuesday, April 17, 2012

FC KILIMANJARO KESHO INAJITUPA UWANJANI KUANZA LEAGUE

Team ya Fc Kilimanjaro kesho siku ya jumatano tarehe 18-04-2012 inaanza kwa kutupa karata yake ya kwanza toka isajiliwe rasmi ktk league daraja la chini hapa sweden.Fc Kilimanjaro itakipiga katika uwanja wa knutby bp,rinkebysvängen saa mbili usiku(20:00)Wachezaji na mashabiki mnaombwa kufika mapema.

AHMED OSAMA UPO WAPI KAKA YANGU?

Kama sijakosea ilikua mwezi wa kumi na mbili 2010 mara ya mwisho kukutana na huyu mtu ndani ya ndege,tena hakuna aliomwambia mwenzie anasafiri duh noma.mpaka leo sijamuona inakua ni nini kaka tutafutane mkubwa.

Sunday, April 15, 2012

KILI MUSIC AWARDS 2012 KATIKA PICHA

                             Ally Kiba akitoa shukrani baada ya kupokea tuzo akiwa na dada yake

                              Ma mc Millad ayo na Vannesa


                                            Quen Darlin akipokea tuzo yake
    Wimbo bora wa ragga ulikwenda kwa arusha gold
 Hapa mwanangu wa ukweli Tito kutoka southafrica akishow love na tuzo ya arusha gold
    Tito na Rama walishafiri kutoka Pretoria SouthAfrica kuja Bongo kushuhudia tuzo za kili 2012
    Babu Tale alipokea tuzo kwa niaba ya Suma Lee na wimbo wake Hakunaga
                       Roma mkatoliki  akionyesha tuzo yake ya wimbo bora wa hiphop
    Ommy Dimpoz akipokea tuzo ya msanii anaechipukia kwa nyimbo yake ya nai nai.

 AT nae akipewa tuzo kwa nyimbo yake vifuu tundu akiwabwaga mahasimu wake offside trik
   Aisha mashauzi nae akua nyumba kwa kukamata tuzo kwa nyimbo bora ya taarab
    Lwiza Mbutu aliiwakilisha Twanga pepeta a.k.a bendi ya watoto wa mjini