Monday, October 29, 2012

HILI NI TANGAZO KWA WALE WATZ WOTE MLIOZOEA MATRAIN HUKO NCHI ZA NG'AMBO,BONGO PIA USAFIRI WA TRAIN KTK MKOA WA DAR UMEANZA RASMI

                                     Train likichanja mbuga katikati ya jiji la Dar
                  Na vituo vikiendelea kutengenezwa ili usafiri kua bora zaidi na zaidi.
     Hapa wakaguzi wa tiket wakiwa kazini kuakikisha hakuna bule lazima ulipe nauli.
 Mandhali mazuri kabisa ndani ya train,seat ndio vile vile kama za matrain ya ulaya wadau.

Hakuna kusukumana wala nini na gazeti unasoma,haya ndio maendeleo tuliokua tunayaota kila kukicha nchini kwetu.Ila mnatakiwa kujua hii kwa wale waishio Dar tu mikoa mingine itafata taratibu.

BAADA YA KUIACHA SWEDEN MIAKA 6 ILIOPITA KICHOCHI AAMUA KUJA KUTUTEMBELEA NA MARA MOJA KABLA AJARUDI DAR

                       Nikaona si mbaya kama nitapata picha nae ya pamoja home boy.
 Kama kaiwaida unapofikiwa na mgeni ni wajibu kua nae kila kona ya mji ili hata akirudi nyumbani aseme alikarimiwa vizuri alipokua Sweden.

     Katikati ya jiji kama kawaida na ubusy wake na sisi tuliendelea na yetu bila hofu.

                                      Pozi katikati ya jiji la Stockholm
 Baada ya mizunguko mirefu nikaona si vibaya tupate chakula na stori za hapa na pale ili kujua Dar wanasemaje.Hii inatokea kwa kila mtu anapofikiwa na mgeni na wewe umeiacha nyumbani muda kidogo,unataka kujua kinaendelea nini?Na nikajibiwa vizuri kwamba bongo raha tu na ndomana yeye akaamua abadilishe upepo na kututembelea sweden na baadae kwendelea na safari zake ndani ya ulaya.

 Kama unavyojua unapokwenda mbali na nyumbani lazima unahakikisha haurudi mikono mitupu, na si kama zawadi kwa ajili ya wenzako au wewe mwenyewe akaamua kutungua vifunika kichwa
 Hapa nilicheka sana akaniambia bongo kaka kinachonikera ni vitu vingi vyakichina.Sasa wacha nichukue simu moja ambayo haijachakachuliwa kwa ajili ya kutumia.Nikamwambia kama umeweza kututembelea utashindwa kununua simu kazi kwako akabeba.
Hapa tukaona tusepe haya maeneo si yakukaa tena.Nashukuru ndugu yangu kwa kunitembelea sina zawadi yakukupa upeleke nyumbani ila ni ujumbe tu waambie hivi.Wasichoke kuniombea kwani nipo katika vita ya maisha na sikujua kama wanadamu pia wamo katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ili kurudishana nyuma sema wasikonde nitarudi na ushindi.Wasalimie wanangu wote kitaani bila kumsahau bibi yangu alionilea kwa moyo wake wote na mpaka sasa nimekua jembe la maana full mashuti na michezo yetu ya hatari.

Sunday, October 28, 2012

MSWAHILI AACHI ASILI!MNYAMA DIAMOND ALA SIKUKUU YA EID ALIKOZALIWA TANDALE

 Huu hapa mkoko wake  baada ya kutumia nyumbani kitambo,nimeipenda sana hii style yake hata nimeamuakuziomba pic hzi kutoka kwa web yake sababu zimenigusa moyoni kwangu.Kiukweli mm pia nimetokea maisha ya chini sana na mpaka hapa nilipo Alhamdulillah kwa kidogo nilichojaaliwa.
 Kitu chakunawa mikono ili kipigwe champunga,asikwambie mtu kuna raha yake kukumbuka ulipotoka,sio kuna wengine wanaona noma mbele za watu kujulikana kama walipotokea choka mbaya nakujifanya wao wamezaliwa matajiri tu mpaka wanakufa.
 Uswazi hakuna mambo mengi  sahani za msosi tunaweka chini na tunapakanyaga na wala hatuumwi kazi kwenu wamasaki kila kitu mnaweka juu sisi kwetu urembo.
 Mpango mzima dah hii hata mm inabidi nifikilie kuandaa same ili nirudi nilipotokea kwani itanifanya nizidi kupata nguvu ya kutafuta na kutojikwanza na kuwaona masikini ni wazembe wakutafuta.Ndevu amepewa mbuzi ww na mdogo na ng'ombe ametoswa na god hakumpa kitu gani.
 Asikwambie mtu bana kuna raha yake hapa ww ambae hujawahi kupitia maisha ya hali ya chini kma sisi huwezi jua,tuachie sisi watoto wa uswazi.
 Mamaaa mwenyewe akose tena anabana mpaka kivuli Wema Sepetu kaungana na mzee amakweli mapenzi msiingilie mtakuja kupata aibu siku moja hawa hapa tena sasa tazama picha inayofata nn Diamond anafanya ndio utaamini hawa wanataka tuamini picha ya jiko bakuli.
 Chukua fanta wema wangu weee hata kama ukiwa na mbili si mbaya ilimradi tu tunywe rangi zakkufanana.Diamond akimpa soda wema.
 Hapa imeshafika na Wema kaipokea sasa tuambieni huyo Jokate yupo wapi hapa?Waacheni bana watu wanaopendana wakiachana hata nyinyi hamtojua,mkijua mjue sio kweli mnazungushwa nyie vichwa vyenu tu wao wanago.
Mama Diamond na wadau wengine.
Picha kwa hisani ya Diamond mnyama thisisdiamond.com

Sunday, October 21, 2012

LORD EYES WA NAKO 2 NAKO AIBA VIFAA VYA GARI YA OMMY DIMPOZ NAKUIACHA FUVU

 Hapa Lord Eyes akipewa kichapi kidogo baada yakukamatwa kwa wizi huo wa vifaa vya gari ya Ommy Dimpoz.Dah kwa kweli inatia aibu na kuhuzunisha kwa msanii kioo cha jamii kama huyu kuwa mwizi.Sijui nini kimemsibu huyo mtaalam wa Hip Hop ya bongo.
                           Hapa gari ya Ommy Dimpoz ikiwa imebakizwa fuvu na mzee mzima Lord Eyes.
                         Hapa akiwa aamini kama amekamatwa dah noma mzee,punguza madawa urudi kwenye game upige pesa kibaji unacho mtu wetu.
                     Hapa akificha sura yake kukwepa camera lakini zimempata unacheza na camera wewe.

Friday, October 19, 2012

TAJIRI EDDY MAPUMZIKONI KWA OBAMA(U.S.A)

 Kiukweli mimi napenda sana nikimuona mtu maisha yake yanamuendea vizuri hasa yule wakaribu yangu kama huyu jamaa.Hii inanifanya kupata chachu ya maendeleo ili kukaza buti katika kutafuta na si kuanza kumuombea mabaya mwenzangu.Mungu aniepushie roho hiyo amen.
 Hapa ndio anapopumzisha mbavu zake Tajiri Eddy baada ya mizunguko ya siku nzima kwenye mapumziko yake huko marekani.
 Nyumba ambayo anapumzika kwa kipindi yupo marekani.Dah nyumba safi sana haya ndugu yangu kula raha a.k.a kula bata swahiba.
                        Tajiri Eddy akiwa amepoz kwenye mpira wa hatari.
 Hapa inakuaje Tajiri ulikwenda madukani kupata mahitaji kidogo?Maana hili pozi ni lakuondoka.


 Tajiri leseni unayo huko au ndio unatumia yakikwete?au ndio kama ile kawaida yetu kuzaliwa Dar form 4, sasa ukisoma unakua full maujanja.Najua huko askari wa tigo wakuwalinda buku tano hakuna kaka kua makini sheria msumeno huko.

 Kama sijakosea hii gari ni Nissan Almada ya 2012 imesimama sana mpaka bei yake,ebu fanya uishishe bongo mzazi tubuluze zile wish na pajero zetu tuzipe likizo kidogo.
Sasa sijui ipi kati ya hii nyeupe na hyo nyeusi utaiangusha bongo,ila jipange ushuru wanaumiza hao mh.Tajiri yangu mm nakutakia mapumziko mema na urudi nyumbani salama kusaka madini kama kawaida maisha yaende amen.Sisi wadau wa sweden tunangoja zawadi utakapokuja huku maana takwimu inasema unatembea sana angani kuliko ardhini.