Wednesday, February 29, 2012

SIKU MASHABIKI WA MPIRA WA MIGUU WALIPOKOJOLEA MASINKI YA KUNAWIA BAADA YA CHOO KATIKA UWANJA MPYA WA TAIFA

                                     Mh kweli sisi bado sana na itachukua muda kuamka

SIJUI LINI BINADAM ITAGUNDULIKA HAKI YAKE TANZANIA

Askari wa FFU a.k.a fanya fujo uone wakiwa wamembeba juu juu kama gunia la chumvi mwananchi na ambae ndio mmiliki wa ardhi ya Tanzania,lakini hapa inaonekana kama amefanya kosa kua nchini kwake.Kiukweli mimi kwa upande wangu hawa askari siwapendi saaaaaaaaana tena zaidi ya sana wao wanachojua ni kumpiga raia sasa sijui ndio sheria ya nchi inasema hivyo!
Sio hawa tu hata wale polisi wanaoitwa wakulinda usalama wa raia hii tafsili haipo  sawa na wafanyacho hawa jamaa wewe muulize mtu yeyote ambae akimuona polisi roho inamuenda mbio au inapoa baada ya kumuona polisi wa tz?atakupa jibu zuri.Lakini hii ni tofauti na nchi za wenzetu polisi anapokuja usoni kwako hata kama unakosa anazungumza vizuri na wewe na mnaelewana na muda mwingine mnataniana sasa jaribu wewe kumtania afande Mwita uone chamoto.

100 NDIO WALIORUDISHA FOMU ZAKUSHIRIKI BIG BROTHER KATI Y A 500 WALIOCHUKUA FOMU


Muda wa kuchukua na kurudisha fomu tayari umekwisha feb 27, na idadi ya watanzania waliorudisha fomu mpaka sasa imetajwa kuwa ni 100 kwa Dar es salaam pekee.
Barbara Kambogi afisa uhusiano wa multichoice Tanzania amesema Kama bado hujajaza fomu na unataka kushiriki, usipate tabu siku za usaili unaweza kwenda hata kama hujajaza fomu na utaingia kwenye usaili kama kawaida, kama walivyoingia waliojaza fomu.
Shindano la big brother afrika mwaka huu linaanza may 6 ambapo ni lazima watu waende wawili wawili, unaweza ukaenda na mama yako, mpenzi wako, mume wako, mke wako, binamu, rafiki au yoyote mwingine.
Swali moja ambalo nilikua na kiu nalo, na nimepata jibu lake ni kuhusu watu waliorudisha fomu wamejaza kina nani watakaokwenda nao?
Watu wengi wamechagua kwenda na rafiki zao tu, wengine magirlfriends zao, wanaofata ni boyfriends, wengine wamechagua ndugu zao kama binamu ila wazazi kama mama sijaambiwa kabisaaa.
Kuna Dola laki tatu, jiulize ukishinda hizo pesa utafanya nini ? ni hela nyingi sana

Saturday, February 25, 2012

BIBI CHEKA FT MH.TEMBA-NI WEWE

VIRUSI HATARI ZAIDI YA UKIMWI


 WANASAYANSI nchini Uholanzi wametengenezea virusi vinavyotishia kuua nusu ya watu duniani kote, vinavyoelezwa kuwa ni hatari zaidi ya vile vya Ukimwi.
Kwa mujibu wa habari zilizoenea duniani kote hivi karibuni zilizofichuliwa na Gazeti la Corriere della Sera la nchini Italia, Kituo cha Tiba cha Erasmus cha Uholanzi ndicho kilichohusika na utengenezaji wa virusi hivyo vya kuambukiza vinavyoweza kuua kwa kasi ya ajabu.
Gazeti hilo liliandika kuwa, utengenezaji huo uliokamilika mwishoni mwa mwaka jana uligundua kuwa virusi hivyo ni aina ya virusi vya mafua ya ndege vya H5N1 na kwamba vina uwezo wa kuambukizwa kwa njia ya hewa kwa mamilioni ya watu.
Mtaalamu wa Kituo cha Tiba cha Erasmus cha Uholanzi, Ron Fouchier alisema kuwa kirusi hicho kimepatikana kwa kufanya mabadiliko katika kirusi cha H5N1 (kile cha mafua ya ndege).
Ron aliongeza kuwa virusi hivyo ambavyo ni aina ya bakteria wanaohifadhiwa kwenye chupa ni miongoni mwa virusi hatari zaidi ambavyo vimekwishatengenezwa hadi sasa.
Utengenezaji wa virusi hivyo umezusha wasiwasi mkubwa huku wataalamu wakihoji hekima na sababu ya kupoteza mamilioni ya fedha kwa ajili ya ishu hiyo ambapo makundi ya kigaidi kama Al-Qaeda, Al-Shabaab na Boko Haram yakiinasa, yatamaliza watu duniani.

Tuesday, February 21, 2012

TAARIFA YA KISOMO CHA MAREHEMU KAKA YAKE SALIM SUPER.

ASALAAM ALAYKUM PANAPO MAJAALIWA YA MUNGU SIKU YA JUMAMOSI 25-02-2012 SA KUMI KAMILI JIONI KUTAKUA NA KISOMO CHA KUHITIMISHA MSIBA WA KAKA YANGU MPENDWA ALIOFARIKI SIKU ZA KARIBUNI NA KUZIKWA NYUMBANI (BONGO).

KISOMO KITAFANYIKA RINKEBY KATIKA UKUMBI WA VISBYRINGEN 6 KARIBU NA BHAI BHAI LIVS.NAWAOMBA NDUGU ZANGU WOTE KWA UJUMLA MJITOKEZE KWANI KUJA KWAKO NDIO KUFANIKISHA KWA HITMA HII.NA KWA WALE MSIOJUA SEHEMU HIYO UNAWEZA KUNIPIGIA SIMU NAMBA 0760984433 NITAKUELEKEZA.NAOMBA UTAKAPOPATA TAARIFA HII MFAHAMISHE NA MWINGINE.
WABILLAH TAWFEEQ.

Sunday, February 19, 2012

MAMA ASUMBULIWA NA UGONJWA HUU KWA MUDA WA MIAKA 12 HUJAFA hujaumbika ni usemi wa wahenga wetu lakini umetumiwa tena na mwanamke Beatrice  Emmanuel Kantimbo (48), ambaye anaumwa ugonjwa wa ajabu uliosababisha  mguu wake kuvimba kwa takribani miaka 12 sasa.
Beatrice almaarufu MC Kimbaumbau, mkazi wa Kibamba wilayani Kinondoni yupo kitandani akiwa hajui hatima ya maisha yake kutokana na tatizo alilonalo la kuvimba mguu. 
Akisimulia tatizo lake, Beatrice anasema:
“Nilianza kuumwa mwaka 1998, nilikuwa na shughuli zangu ambazo zilikuwa zikiniingizia kipato na kunifanya nimudu kusomesha watoto wangu.
“Tatizo la kuumwa mguu lilianza wakati natoka kazini, nilisikia kitu kama ganzi katika mguu huu wa kulia na baadaye ikaja homa kali, kitu ambacho kilinishangaza sana kwani sikuwahi kuumwa hivyo.
“Nilikwenda kutibiwa katika hospitali moja iliyopo Kimara na wakati nikiwa kituoni kusubiri usafiri, mguu ulianza kuvimba, hali ambayo ilinifanya nifikirie kuwa ni masuala ya kishirikina.
“Nilipofika nyumbani, baada ya siku chache mguu ulianza kutoka malengelenge kama mtu aliyeungua moto na ndipo vidonda vilipoanza kutoka.
“Nilipelekwa Hospitali ya Hindu Mandal kutibiwa  vidonda hivyo lakini baadaye hali ilizidi kuwa mbaya hadi ndugu zangu wakaamua kunipeleka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Madaktari katika hospitali hiyo, baada ya uchunguzi waliniambia mishipa inayotembeza damu mguuni imeziba lakini mfupa wa ndani uko salama.
“Kwa sasa siwezi kujishughulisha na chochote, huwa nalala tu, nikikaa nasikia maumivu makali sana, hakika sina raha ya maisha.  
“Nimetibiwa sana sehemu mbalimbali lakini sipati nafuu, mawazo yangu sasa ni kwenda India kutibiwa lakini niliambiwa gharama yake ni shilingi milioni 45, yaani nauli na matibabu. Fedha hizo ni nyingi sana, mimi na ndugu zangu hatuna uwezo.
“Nina mtoto wangu ambaye alikuwa kidato cha pili, ameshindwa kwenda shule kwa kuwa sina fedha za kumlipia ada, hivyo tatizo hili limezaa tatizo lingine.
“Hivi sasa mtoto huyo kazi yake kubwa ni kuniogesha na kunipikia chakula kinapopatikana na kama hakipo tunalala njaa.
“Nawaomba Watanzania wenzangu wanisaidie kunichangia chochote. Naamini kwa msaada wao nitaweza kupelekwa India na kutibiwa hadi kupona kwa sababu madaktari wa Muhimbili wamenithibitishia kuwa mfupa wangu ni mzima kabisa. Naumia sana mwenzenu,” alisema mama huyo huku akitokwa na machozi.
Mtu yeyote aliyeguswa na habari hii na anahitaji kumsaidia, anaweza kuwasiliana kwa simu yake namba 0716 850 350 au kutumia chochote kwa Tigo Pesa au kwa kutumia akaunti ya CRDB Namba 0112003893000 Blandina Julius- Mhariri.
                        Kwa hisani ya globalpublishers.

MAWAZO JUU YA WANAUME NDIO YALIONIINGIZA KATIKA USAGAJI-JINI KABULA

Msanii aliyeibuka kwenye tamthilia Miriam Jolwa ,Jini Kabula anaelezea sababu iliomfanya kuingia katika usagaji ni mlundikano wa mawazo alioupata kutokana na kutendwa na wanaume.Kiukweli wanaume mda mwingine wanaweza kua chanzo cha wewe kufanya mabaya hasa baada ya kukuumiza.Ndio niliingia ktk huu mchezo kwangu ilikua ni kimbilio langu la kutoa mawazo kwa kutendwa na wanaume wa mjini hasa hapa dar,lakini namshukuru mungu kwa sasa nimeacha hili swala na nimemrudia mungu wangu kwani nilikua namkosea sana natumaini atanisamehe kwani mimi binadam nisiekamilika.

Saturday, February 18, 2012

WITNEY HOUSTON AZIKWA LEO

                                        Jeneza la witney houston
                                                         Gari iliobeba mwili wa Witney
 Mume wa zamani wa Witney Bob Brown akiingia ktk gari yake na kuondoka sehem ya kanisa ambapo aliagwa mzazi mwenzie huyo.Mshkaji alishindwa kuingia kanisani kwani familia haikumtaka awepo ktk mazishi ila kiubishi aliudhulia nje na bdae kuondoka.

              Hapa Boby Brown akiwa ktk sura ya huzuni nje ya kanisa aliloagwa mama mtoto wake Witney

TUNDAMAN A.K.A CAPTEN HAPA KABILA FULANI UMEWAKAMATA.

Monday, February 13, 2012

HAPPY BIRTHDAY TO YOU NAGMA

TATOO ZA LULU ZAWASUMBUA MAPEDESHEE WA DAR

UKIONA MATESO YANAZIDI JUA UKOMBOZI UPO NJIANI

DAR LIVE YAZIDI KUWASHA MOTO KILA SIKU

                             MSHIRIKI WA IMBA,VAA,CHEZA KAMA RIHANNA
                 AY  NA MWANA FA WAKIKAMUA VILIVYO NDANI YA DAR LIVE

                         TWANGA PEPETA KISIWA CHA BURUDANI WAKIKAMUA
                                 WASHILIKI WA IMBA,VAA,CHEZA KAMA RIHANNA
                                 WATOTO WA KIUMENI WAKIKAMUA UWANJA WA NYUMBANI
                                             DOGO ASLEY WA KIUMENI

TUNDAMAN ALIVYOPELEKA BURUDANI YA MANZESE UINGEREZA

                                   TUNDAMAN A.K.A CAPTEN
                                   WALIPAGAWISHWA NA NGOMA NA MANZESE
                                     MAUA YALIKUA MENGI SANA

JAY Z NA BEYONCE WAANIKA PICHA ZA MTOTO WAO

                                                 BLUE IVY CARTER
                                       JAY Z AKIWA NA MWANAWE
                                           MAMA NA MWANA

LADY IN RED RELOADED ILIVYOFUNIKA PICHA ZINASEMA

Saturday, February 11, 2012

TAARIFA YA MSIBA

NDUGU SALIM(SUPER)ANAWAPA TAARIFA YA MSIBA WA KAKA YAKE ALIOFARIKI NYUMBANI(TZ)JUZI NA KUZIKWA JANA.KAMA KAWAIDA YETU MWENZETU ANAPOFIKWA NA TATIZO KAMA HILI NA LINGINE NIWAJIBU WETU KUMKIMBILIA NA KUMFARIJI.

KWA WALE AMBAO WATAPATA NAFASI YA KWENDA KUMPA POLE NDUGU SALIM SUPER UNAWEZA KWENDA ANAPOISHI RINKEBY NYUMBANI KWA SHEKH JUMA,NA KWA WALE WANAOWEZA KUMPA POLE KWA SIMU UNAWEZA KUMPIGIA KWA SIMU YAKE NAMBA 0760984433.

DARSTOCKHOLM NA WADAU KWA UJUMLA INATOA POLE KWA SALIM SUPER,MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEMA AMEN.