Wednesday, February 29, 2012

SIJUI LINI BINADAM ITAGUNDULIKA HAKI YAKE TANZANIA

Askari wa FFU a.k.a fanya fujo uone wakiwa wamembeba juu juu kama gunia la chumvi mwananchi na ambae ndio mmiliki wa ardhi ya Tanzania,lakini hapa inaonekana kama amefanya kosa kua nchini kwake.Kiukweli mimi kwa upande wangu hawa askari siwapendi saaaaaaaaana tena zaidi ya sana wao wanachojua ni kumpiga raia sasa sijui ndio sheria ya nchi inasema hivyo!
Sio hawa tu hata wale polisi wanaoitwa wakulinda usalama wa raia hii tafsili haipo  sawa na wafanyacho hawa jamaa wewe muulize mtu yeyote ambae akimuona polisi roho inamuenda mbio au inapoa baada ya kumuona polisi wa tz?atakupa jibu zuri.Lakini hii ni tofauti na nchi za wenzetu polisi anapokuja usoni kwako hata kama unakosa anazungumza vizuri na wewe na mnaelewana na muda mwingine mnataniana sasa jaribu wewe kumtania afande Mwita uone chamoto.