Saturday, April 7, 2012

STEVEN KANUMBA AFARIKI DUNIA,POLENI FAMILIA POLENI WATANZANIA

 Ama kwa hakina nilipoipata habari hii usiku mkubwa sikuamini nikaona kama naota juu ya kifo cha mcheza filamu mkubwa Tanzania na africa Steven Kanumba.Ukweli niliouakikisha ni kwamba steven kanumba ametutoka duniani,chanzo cha kifo chake inasemekana Steven kanumba alikua na mahusiano kimapenzi ya siri na mcheza filamu mwenye umri mdogo Lulu Michael ambapo jana usiku akiwa nyumbani kwake sinza alikua anajiandaa kutoka out ndipo ukatokea mlumbano baina ya yeye na Lulu chumbani kwa Kanumba ndio Lulu alipomsukuma Kanumba.Gafla Lulu akitoka chumbani kwa Kanumba akaenda kumfata mdogo wa kanumba na kumwambia akamtazame kanumba ameanguka na anatoka damu,ndipo  mdogo wa Kanumba alikwenda kumtazama kaka yake kweli ameanguka na anatokwa na damu ndio akaenda kumwita daktari wa Kanumba kurudi nyumbani Lulu alikua ameshaondoka .Maiti ya marehemu kanumba kwa sasa ipo hospitali ya taifa ya muhimbili na Lulu ameshakamatwa na Polisi yupo katika kituo cha polisi Osterbay kwa maelezo zaidi.
 Msanii Jackline Wolper akiwa amezimia kwa mstuko wa kifo cha Kanumba,ikumbukwe Kanumba alikua ktk matahalisho ya mwisho ya filamu yake ya ndoa yangu wakiwa pamoja na Jacline Wolper.
                                      Vilio vilitawala nyumbani kwa Kanumba
                                        Waombolezaji wakiwa ktk huzuni
                                    Wema Sepetu wa akiwa aamini kilichotokea
 Huu ni umati wa watu uliofika nyumbani kwa Kanumba juu nini kimejili juu ya kifo cha kipenzi chao Kanumba.
                                    Waandishi wa habari walikuwepo kupata habari
Mdogo wa Kanumba akitoa taarifa ya kifo cha kaka yake kwa vyombo vya habari.Nikiwa kama Mtanzania na Shabiki wa Steven Kanumba nimepokia kifo hiki kwa masikitiko makubwa sana.Ila yote ni yote Mungu amlaze Steven Kanumba mahala pema amen.Kila nafsi itaonja umauti duniani tunapita.