Wednesday, April 4, 2012

DIAMOND NAE AVUNJA UKIMYA JUU YA MANENO YA WEMA.


 kiukweli mimi sipendi ugomvi, na haya nisinge yasema kama yeye asingekuja kuongea uongo, yani hata sababu kubwa ya mimi na yeye kutofautiana ilikua ni kitu kidogo tu anakipeleka kwenye media na ikafika time anasema hanitaki ila mimi ndio namng’anga’nia wakati ukweli ni kwamba alikua analetwa nyumbani na rafiki zake na ndugu zake akilia anaomba isuluishwe turudiane, mpaka anampigia mama yangu mzazi, rafiki zangu na ndugu kama Shetta na Romy Jones, pia anawaambia marafiki zake waandae sehemu ya Dinner ili atokee kama Suprise”
Diamond amesema “kabla ya show yangu ya juzi alikuja nyumbani mimi niko ndani navaa nasikia sauti yake barazani, namuuliza ndugu yangu Rommy ananiambia ni Wema, nauliza kafata nini nyumbani? mimi nina mpenzi wangu na yeye anamfahamu na hizi drama za Wema zinafanya mpenzi wangu akasirike kwa sababu anaona bado naendelea na Wema, sasa pale nyumbani nilitoka nje baada ya kukasirika ila wakanishika nisimguse, ndio wakamwambia aondoke… yani baada ya kugundua kwamba mimi sitaki kuwa na yeye tena sasa anatumia kama ile hautaki kuwa na mimi, Nakuharibia sasa”
“Wakati anakuja kunipa hela kwenye stage mi nilikua naogopa kwa sababu tayari alikuja nyumbani kabla yake ndio maana nilihisi anataka kufanya drama nyingine tena ndio maana nikamkwepa na kujifanya kama sijamuona lakini akaganda makusudi kama anataka kufanya kitu flani, mpaka mwisho baadae akamfata Q Chief anamlilia pia kawafata mama yangu na mama mdogo anawaambia mimi mtoto wenu nampenda sana ananitesa, alafu baada ya hapo anakuja kwenye Media na kuongea vitu vingine, na kunitengenezea mazingira ili mimi nionekane mbaya” – Diamond
Katika sentensi nyingine Diamond amethibitisha kwamba kwenye  hiyo show yake kulikua na wasichana wawili ambao waliwahi kuwa wapenzi wake, na walijitokeza pale kwenye stage na kumpa pesa na yeye alizipokea bila tatizo kwa sababu hana tatizo nao akiwemo Sarah ambae nlimwimbia “Nenda kamwambie” ila za Wema alizikataa makusudi kwa sababu alikua anataka kutengeneza drama manake ishu isingeishia pale.
Platnums ameizungumzia ishu nyingine kwamba “hata nilipokua kwenye uhusiano na yeye nilishawahi kumuonya Wema mara nyingi, niliku sipendi kuwa na mtu anaeandikwa andikwa sana kwenye magazeti, kabla nilijua ni umaarufu lakini nikagundua kwamba alikua anazipeleka stori mwenyewe tena na hela ya kuwalipa waandishi anatoa, na kuna kipindi nililipa hela waandishi wasiandike hizo habari lakini Wema akatoa zaidi ya hiyo, alikua anapeleka stori mwenyewe, kama juzi alisikia naumwa niko hospitali akanipigia kunipa pole…. kesho yake nikaona stori kwenye gazeti wakati hakuna aliefahamu zaidi yake na stori imetoka vilevile, nikakasirika sana”
“katika tukio lililoniudhi zaidi ni pale nilipogundua alipopeleka stori ya kuniharibia kwenye gazeti kwamba nina nuski na ishu nyingine kibao, baada nikakutana nae nikamuuliza kwanini unapeleka hizo habari kwenye gazeti? akazuga kwa kumpigia simu mwandishi na kuanza kumtukana mbele yangu kwamba hizo habari ameandika tofauti, sio kama alivyomuhoji, lakini baadae wakati nimeondoka alimpigia simu na kucheka huku akimwambia tumemuweza leo, Wallah nimlale mama yangu mzazi hicho kitu ndio kiliniuma nikaona bora tuachane kwa sababu niligundua ananitumia mimi kufanya mambo yake, amesema yeye ndio alianza kuwa staa kabla yangu….. ni sawa ila mimi kuanza kwangu nimekuja na akili, yeye anataka kutumia wanaume mastaa apate umaarufu”
“Kilichonifanya nijue kwamba amenizunguka kwenye ile habari ni wakati nilipokutana na huyo mwandishi ambae alinithibitishia kwamba Wema mwenyewe ndio aliipeleka ile habari na kweli baada ya kunizuga kwa kumtukana, alimpigia simu mwandishi na kucheka baada ya mimi kuondoka” – Diamond
“Niliamua kuwa kwenye mapenzi na Wema na kujipa moyo kwamba nitairekebisha tabia yake, na nilikua napigiwa simu na watu mbele yake wakiniambia ananiharibia nyota mpaka analia yani, nikawa namsafisha kwa watu kwamba hayuko hivyo mpaka watu wakaanza kupenda uhusiano wetu, kumbuka baada ya yeye kuachana na Kanumba alikimbia kwenda Marekani, akarudi tena bongo na kuanza kunitongoza kwenye facebook kwa sababu alikua anajiuliza ataanza kutoka na nani ili azidi kupata umaarufu” – Diamond
Leo kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM Diamond ataendelea kufunguka Exclusive mambo mengine hakutaka kuyasema kwenye Media lakini imebidi kwa sababu Wema ameshindwa kujiheshimu na kutaka yeye aonekane mbaya, atataja pia moja kati ya tukio la ajabu alilowahi kulishuhudia kwa Wema lakini hakulisema wala halikuharibu chochote kwenye uhusiano wao, Diamond atafunguka pia kuhusu rekodi ya Mauzo aliyoivunja kwenye show ya Mlimani City.Stori kutoka kwa millard Ayo.