Thursday, November 3, 2011

BREAKING NEEEEEWS MIMI NA MSHKAJI KWA SASA PAMOJA TUNAWAKILISHA AMANI NA UPENDO

 Kiukweli katika jambo ambalo najihisi shujaa mbele ya mungu ni hili tukio nililolifanya siku ya juma3 kwa kukutana na ndugu yangu Abdallah a.k.a Dullah kumaliza tofauti zetu zilizodumu muda mrefu kama sikosei miaka 5,kiukweli namshukuru mungu mshkaji mwelevu alinielewa mara moja.Kwanza tumetoka sehem moja kiumeni pili maskani moja tatu kaka yake na baba yangu walianza safari za kutafuta maisha pamoja nje ya Tanzania miaka ya 80.

Wadau wangu nitawaomba radhi  kwa namna moja au nyingine kama nimewakwanza kuweka taarifa hii lakini kwangu nimeona ni hatua kubwa nilioifanya ndio maana nikaona nitundike.Kiufupi sina haja yakueleza tatizo lililopelekea kukosana na ndugu yangu huyu miaka 5 iliopita nafanya hivi sababu inaweza kua nimemkwanza mtu mmoja au mwingine na mimi sio lengo langu kumkwaza mtu kupitia blog yangu.