Sunday, March 25, 2012

BURGER NI CHAKULA KINACHONIFANYA MPAKA SASA NIWE STOCKHOLM

Wadau wangu hii ni burger aina ya big mac nimeitengeneza kwa mkono wangu mwenyewe.Kiukweli kwako itakua inaleta maana kama chakula tu ila kwangu mimi ni tofauti kabisa na inamaana kubwa sana kwani ndio utengenezaji wa hii na zingine ndio zimenifanya niwepo hapa Sweden sijui nini kingetokea kama isingekua hii.Kuna mengi sana ktk maisha ya mwanadam mpaka kufikia mafanikio kuna vikwazo vya kila aina na hata wanadam wanaweza kuwa mstari wa mbele kuakikisha usifikie mafanikio yako ila hii burger imenifanya niwe strong,najiamini,siogopi kitu wala mtu zaidi ya mungu.Mimi sitaki kumaliza yote kuhusu burger juu ya maisha yangu ila naikubali sana na najivunia kwa mengi niliofanya kutokana na mkono wangu kuweza kuitengeneza hii tu.