Tuesday, March 20, 2012

MACDONALD MARIGA AANZA KUTUMIA PESA ZAKE KWA MAGARI YAKIFAHARI

 Kiukweli siku zote naechumia juani ipo siku atakula kwenye kivuli.Si msemo huo tu pekee hata mda mwingine waswahili wanakwambia mateso yakizidi jua ukombozi upo njiani na pale ukombozi unapokufika hakuna anaejua kama ulipata mateso katika kutafuta kwako.
 Hii inaonyesha wazi kwamba Macdonald Mariga amepitia mengi sana katika mbio zake za maisha katika mpira wa miguu.Na bila kupinga kwa sasa ndio anakula akiwa kivulini kama unavyoona magari anayoendesha kwa sasa.
Kiukweli hii inaweza kuleta chachu hata wachezaji wetu wa Tanzania kupatwa na uchungu juu ya maendeleo ya mchezaji mwenzao ambae ameanza kwa kiwango kama chao na kwa sasa yupo juu na hata dunia inamtambua na kumuheshimu.Sasa kazi kwenu wachezaji wetu wa Bongo kukaza buti ili kufika hatua ya mchezaji mwenzenu Mariga.