Wednesday, March 21, 2012

NYUMBA YA SPIKA WA BUNGE IMEGHARIMU TSH BILION 1,5

Hatimaye Spika wa Bunge la Tanzania pale Dodoma atakuwa na makazi rasmi baada ya ujenzi wa nyumba ya Spika kukamilika na makabidhiano kufanyika. Nyumba hiyo ambayo ipo maeneo ya Uzunguni nje kidogo ya Dodoma mjini imegharimu takribani Tshs 1.5 Billion na imejengwa na kampuni ya Pacha Building Construction Company. Hii inakuwa nyumba ya kwanza rasmi ya Spika kwani hapo awali hapakuwahi kuwa na nyumba rasmi ya Spika