Monday, September 10, 2012

KILA MBUZI ATAKULA KWA UREFU WA KAMBA YAKE

 Ebana hii ilikua kali kidogo kwangu na watu waliokua wakipita njiani katikati ya jiji la stockholm.Jamaa alikua ameshikilia hiyo fimbo na amekaa juu na hakukua na kitu chochote alichokalia.
 Hii ilifanya kila aliepita pale asimame na kutazama maajaabu hayo na hakuna alielazimishwa kutoa pesa bali alitoa mwenyewe kwa mapenzi yake hii inaonyesha watu wanavyokua na mbinu za utafutaji pesa.
Hapo alikua na mwenzie ambae alikua yupo makini kukataza mtu yeyote anaetaka kukivuta  au kufunua hicho kicapert sasa sijui nini ilikua siri yake hapo,mimi nilichofanya kumpiga picha na kupiga nae picha na kusepa ila sikuunga mimi sababu nilipotea mfukoni.