Friday, October 21, 2011

TAARIFA YA MSIBA

Feruzi Ahmed Said (Mume wa Dorina) amefiwa na baba yake mzazi Mzee Ahmed Said leo alfajiri.

Feruzi anapenda aende nyumbani (Dares Salaam) haraka iwezekanavyo kuhudhuria mazishi kama atawahi. Ikishindikana aende kuhani.

Yeye na mke wake wanaleta ombi la msaada wa hali na mali kwa jumuia ya watanzania ili Feruzi aweze kwenda katika mazishi.

Kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kumfikishia msaada huu kama una uwezo, tafadhali piga simu Na. 0722982865 (Feruzi) au 0737143048 (Dorina).

Kwa wale wataoweza kwenda kuwaona msiba uko, Konsolvägen 7, Hökarängen, (Green Line kwenda Farsta)

Watashukuru sana kwa msaada wenu.


KAMA KAWAIDA YETU MWENZETU ANAPOFIKWA NA TATIZO KAMA HILI NI WAJIBU WETU KUMKIMBILIA NA KUFARIJI,KWANI KESHO ITAKUA ZAMU YAKO WEWE AU MIMI PIA.TUNAOMBWA WOTE KWA PAMOJA TUPATAPO MUDA TUJITOKEZE NYUMBANI KWA MFIWA.