Saturday, October 22, 2011

WEEK TATU ZA KUVISHWA PETE YA UCHUMBA WEMA ABWAGWA NA DIMOND SABABU MAMA WA DIMOND

Msanii wa kizazi kipyaDimond amemtema rasmi mpenzi wake ambae ni msanii wa filamu za bongo Wema Sepetu.Habari zilizosibitishwa na waandishi wa habari ambazo walizipata moja kwa moja kwa mtu mzima Dimond,kweli kabisa ndugu waandishi nimeamua kuwaita na kuwaipa hii taarifa kwamba sipo tena na Wema japo nilimvisha pete week 3 zilizopita.Na sababu kubwa za kumuacha mrembo huyu ni kwamba ampendi mama yangu mzazi na hataki tukae nae pamoja anataka mama yangu nimrudishe tandale mm na yeye tuendelee kuishi Sinza.Kiukweli hili silikubali japo nampenda wema lakini mchezo na mama yangu mzazi sipo tayari kumtelekeza sababu ya mapenzi,kwani hata yeye Wema amesahau kwamba bila mama yangu yeye asingenijua,kwanza mama yangu amenizaa na amenilea kwa tabu baada ya baba yangu kunikataa nimepata shida na yeye mama yangu maisha yetu yote ya dhiki siku tunakula siku tunalala na njaa.Na huyo huyo mama yangu ndio niliomuibia pete yake ya dhahabu nikapata pesa na kwenda kurecord nyimbo na mama yangu akanivumilia na kunipa baraka na mpaka nikatoka katika mziki sasa huu ndio muda wake wakula tunda la mwanae mzeya sasa vipi nimtelekeze sababu ya yeye Wema?sipo tayari kwa hilo ni bora nimuache yeye sio mama yangu nadhani nimeeleweka waandishi.Wema nae alipotafutwa na kupatikana alishindwa kuongelea hili na kusema sipo tayari kuliongea hili sipo sawa kwa sasa nitawatafuta mwenyewe.