Tuesday, June 26, 2012

MSIBANI KUNAPOCHAFUKA NA MAPANGA SHAAA

 Stori nzima ilikua hivi.Nina rafiki yangu wa karibu alifiwa na baba yake mzazi,alinipa taarifa ili nihudhulie mazishi,nilisimamisha pilika zangu na kutokea msibani tayari kwa mazishi nilipofika nilikutana na haya..
 Marehem alikua muislam na akawahi kubadili dini na kua mkristo baada ya kupendana na mwanamke mkristo na akazaa nae mtoto wakiume ambae nae alikua mkristo ila mtoto wake huyo huyo baadae alibadili  dini na kua muislam.Ilipita mwaka mtoto wa marehem alibadili tena na kurudi katika ukristo na mpaka sasa yupo katika imani ya ukristo.
Haikujulikana kama mzunguko huu wa kubadili dini ungeweza kuleta tabu baadae,sasa ikawa kivumbi baba mzazi wa huyu kijana alipofariki kwani mtoto anataka baba yake azikwe kikristo na ndugu wa marehem ambao wote wakristo wanataka ndugu yao azikwe kislam yakaanza malumbano.......
Baada ya muda nikiwa nimejisahau kushika camera walitokea watu kama kumi wakiwa na mapanga na kuanza kuwapiga watu na mabapa ya upanga na wengine kukata tulubai na miti ya tulubai,kiukweli zikaanza mbio za mita mia ila alikosekana usein bolt tu na pia refa hakuwepo.....
mimi pia sikua nyuma katika wakimbiaji ila chakushangaza nilisahau kuibeba gari maana hata magari yalipigwa mapanga.Baada ya muda kukatulia ndio vikaanza vifungu vifungu kujadili lakini wenye mapanga walikaa pembeni na kusema hatutaki msiba ondokeni na jeneza likija hapa tutalivunja.Mpaka naondoka eneo latukio msiba ukavunjwa katika hyo nyumba na mtoto wa marehem akaambiwa atafute nyumba atakayoweka msiba na sio pale nyumba ya waislam aweke msalaba.Dah duniani kuna vituko sana,kesho nitawasiliana na mtoto wa marehem nakujua msiba ulikwenda vipi na walizikaje au bdo marehem hajazikwa?nitawajuza wadau