Wednesday, December 7, 2011

AFA HOTELINI NA AKUTWA NA KETE 60 ZA MADAWA YAKULEVYA


Kete 60 za madawa ya kulevya ambazo zilikuwa mwilini mwa Bushaga Masalai mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa jijini Dar es Salaam ambaye ni mfanyabiashara kati ya Dar es Salaam na Tunduma mkoani Mbeya amefariki dunia akiwa chumba cha kupanga katika Hoteli ya High Class, Tunduma.

Marehemu alifika hotelini hapo Desemba 2, mwaka huu akitokea jijini Dar Es Salaam, lakini Desemba 3, wahudumu walipokuwa katika shughuli zao za usafi katika hoteli hiyo walijaribu kugonga mlango wa chumba hicho alichopanga marehemu, lakini haukufunguliwa kutokana na ukimya huo waliamua kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi majira ya saa 6 mchana.

Hata hivyo Jeshi la polisi mji mdogo wa Tunduma baada ya kupewa taarifa lilifika hotelini majira ya saa 6 na dakika 30 ili kufanya uchunguzi na kisha kuubomboa mlango huo ndipo walipomkuta Bwana Bushanga akiwa amefariki dunia.
Wakati huo huo kete hizo zitasafirishwa kwa mkemia mkuu jijini Dar es salaam kwa ajili ya uchunguzi ili kubaini aina gani ya madawa hayo, pamoja na thamani yake na kwamba shughuli za kusafirisha mwili wa marehemu zitafanyika baada ka kukamilika kwa zoezi la kuwapata ndugu wa marehemu huyo.