Wednesday, December 14, 2011

KAMATA MWIZI MEEEEN,D PLATNUM AGONGANISHA MAGARI

 Habari zisizo rasmi zilizoenea mjini ni kwamba Wema sepetu amjia juu Jokate baada ya kusemekana alivunja amri ya sita wakati wakifanya video ya "mawazo" na Mchumba wa Wema namzungumzia Diamond.
Nyeti zinaendelea kusema Wema alifumania Jokate akibadilisha radha ya ndimi na Diamond,hata hivyo wema alilalama sana kutokana na kumwamini JOKATE  ni rafiki wa karibu asingeweza kumpa mambo Diamond.
 nyeti zaidi...
KISHINDO cha Jokate Mwegelo ni kizito, kimeingia ndani ya uhusiano wa brazameni, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Wema Sepetu kisha kuwafanya wawili hao kila mmoja kushika hamsini zake.
Wema, amefunga virago, ameondoka nyumbani kwa Diamond, Sinza Madukani, Dar es Salaam kwa mtindo wa “wanakwenu kwa heri, nimechoka masimango, narudi nyumbani kwetu leo.”
Madai ‘yanahiti pointi’ kuwa Diamond na Jokate wapo kwenye penzi jipya lenye nguvu, Wema ameligundua hilo, ameona ni maji marefu, kwa hiyo amejiweka pembeni kuepuka msongamano.
Inazidi kudaiwa kwamba Wema alijaribu kumfanya Diamond atulie lakini ikashindikana, ilipodhihirika Jokate ameshika mpini, alianza kupata mateso ya moyo na hisia kwa jinsi alivyofanywa ‘spea tairi’. Madai ‘yanahiti’ pia kwamba Wema alithibitisha kuwa Diamond na Jokate wanamchezea ‘ukuti ukuti’ baada ya kuwafumania wakiwa ‘vere klozi’ kimahaba kwenye Hoteli ya Picolo, Masaki, Dar es Salaam. Hata hivyo, inadaiwa kuwa Wema alipowakuta Diamond na Jokate, hakuangusha varangati kama mmiliki, badala yake alinywea utadhani yeye ndiye mwizi kisha akawaambia: “Samahanini sana kwa kuwaingilia kwenye starehe zenu.”