Monday, October 29, 2012

BAADA YA KUIACHA SWEDEN MIAKA 6 ILIOPITA KICHOCHI AAMUA KUJA KUTUTEMBELEA NA MARA MOJA KABLA AJARUDI DAR

                       Nikaona si mbaya kama nitapata picha nae ya pamoja home boy.
 Kama kaiwaida unapofikiwa na mgeni ni wajibu kua nae kila kona ya mji ili hata akirudi nyumbani aseme alikarimiwa vizuri alipokua Sweden.

     Katikati ya jiji kama kawaida na ubusy wake na sisi tuliendelea na yetu bila hofu.

                                      Pozi katikati ya jiji la Stockholm
 Baada ya mizunguko mirefu nikaona si vibaya tupate chakula na stori za hapa na pale ili kujua Dar wanasemaje.Hii inatokea kwa kila mtu anapofikiwa na mgeni na wewe umeiacha nyumbani muda kidogo,unataka kujua kinaendelea nini?Na nikajibiwa vizuri kwamba bongo raha tu na ndomana yeye akaamua abadilishe upepo na kututembelea sweden na baadae kwendelea na safari zake ndani ya ulaya.

 Kama unavyojua unapokwenda mbali na nyumbani lazima unahakikisha haurudi mikono mitupu, na si kama zawadi kwa ajili ya wenzako au wewe mwenyewe akaamua kutungua vifunika kichwa
 Hapa nilicheka sana akaniambia bongo kaka kinachonikera ni vitu vingi vyakichina.Sasa wacha nichukue simu moja ambayo haijachakachuliwa kwa ajili ya kutumia.Nikamwambia kama umeweza kututembelea utashindwa kununua simu kazi kwako akabeba.
Hapa tukaona tusepe haya maeneo si yakukaa tena.Nashukuru ndugu yangu kwa kunitembelea sina zawadi yakukupa upeleke nyumbani ila ni ujumbe tu waambie hivi.Wasichoke kuniombea kwani nipo katika vita ya maisha na sikujua kama wanadamu pia wamo katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ili kurudishana nyuma sema wasikonde nitarudi na ushindi.Wasalimie wanangu wote kitaani bila kumsahau bibi yangu alionilea kwa moyo wake wote na mpaka sasa nimekua jembe la maana full mashuti na michezo yetu ya hatari.