Tuesday, October 9, 2012

BIASHARA MATANGAZO-MSANII WA FILAMU BONGO AANIKA TATOO ZAKE

 MSANII ndani ya tasnia ya filamu na tamthilia za kibongo Rayuu, azidi kujichora tattoo kwenye mwili wake ambapo sasa aamua kuchora kiunoni na sehemu nyingine nyeti. Mtandao wa DarTalk baada ya kusikia taarifa hizo kutoka kwa rafiki yake kipenzi kuwa msanii huyo amezidi kujichafua mwili kwa kujichora ndipo ulipoamua kumtafuta ili kupata ukweli wa ishu hiyo na alipopatikana alifunguka kuwa ni kweli lakini zote alizochora hazina ubaya wowote.
Rayuu alisema kuwa amechora michoro hiyo sehemu nyingi za mwili wake kuanzia kiunoni, shingoni, kwenye maziwa, makalio na mapaja na alidai kuwa anajisikia furaha kuwa na tattoo hizo kwani hajafanya kwa kushawishiwa na mtu.

Alidai kuwa hata hivyo kati ya michoro hiyo aliouweka kiunoni unasomeka jina lake la ‘Rayuu’ na mengine ni ya aina mbalimbali, “tattoo nazipenda sana lakini kati ya zote hii ya kiunoni naipenda kuliko zote ingawa aliyenichora aliikosea kidogo,” alisema.
KWA HISANI YA DARTALK