Friday, October 19, 2012

TAJIRI EDDY MAPUMZIKONI KWA OBAMA(U.S.A)

 Kiukweli mimi napenda sana nikimuona mtu maisha yake yanamuendea vizuri hasa yule wakaribu yangu kama huyu jamaa.Hii inanifanya kupata chachu ya maendeleo ili kukaza buti katika kutafuta na si kuanza kumuombea mabaya mwenzangu.Mungu aniepushie roho hiyo amen.
 Hapa ndio anapopumzisha mbavu zake Tajiri Eddy baada ya mizunguko ya siku nzima kwenye mapumziko yake huko marekani.
 Nyumba ambayo anapumzika kwa kipindi yupo marekani.Dah nyumba safi sana haya ndugu yangu kula raha a.k.a kula bata swahiba.
                        Tajiri Eddy akiwa amepoz kwenye mpira wa hatari.
 Hapa inakuaje Tajiri ulikwenda madukani kupata mahitaji kidogo?Maana hili pozi ni lakuondoka.


 Tajiri leseni unayo huko au ndio unatumia yakikwete?au ndio kama ile kawaida yetu kuzaliwa Dar form 4, sasa ukisoma unakua full maujanja.Najua huko askari wa tigo wakuwalinda buku tano hakuna kaka kua makini sheria msumeno huko.

 Kama sijakosea hii gari ni Nissan Almada ya 2012 imesimama sana mpaka bei yake,ebu fanya uishishe bongo mzazi tubuluze zile wish na pajero zetu tuzipe likizo kidogo.
Sasa sijui ipi kati ya hii nyeupe na hyo nyeusi utaiangusha bongo,ila jipange ushuru wanaumiza hao mh.Tajiri yangu mm nakutakia mapumziko mema na urudi nyumbani salama kusaka madini kama kawaida maisha yaende amen.Sisi wadau wa sweden tunangoja zawadi utakapokuja huku maana takwimu inasema unatembea sana angani kuliko ardhini.