Sunday, October 28, 2012

MSWAHILI AACHI ASILI!MNYAMA DIAMOND ALA SIKUKUU YA EID ALIKOZALIWA TANDALE

 Huu hapa mkoko wake  baada ya kutumia nyumbani kitambo,nimeipenda sana hii style yake hata nimeamuakuziomba pic hzi kutoka kwa web yake sababu zimenigusa moyoni kwangu.Kiukweli mm pia nimetokea maisha ya chini sana na mpaka hapa nilipo Alhamdulillah kwa kidogo nilichojaaliwa.
 Kitu chakunawa mikono ili kipigwe champunga,asikwambie mtu kuna raha yake kukumbuka ulipotoka,sio kuna wengine wanaona noma mbele za watu kujulikana kama walipotokea choka mbaya nakujifanya wao wamezaliwa matajiri tu mpaka wanakufa.
 Uswazi hakuna mambo mengi  sahani za msosi tunaweka chini na tunapakanyaga na wala hatuumwi kazi kwenu wamasaki kila kitu mnaweka juu sisi kwetu urembo.
 Mpango mzima dah hii hata mm inabidi nifikilie kuandaa same ili nirudi nilipotokea kwani itanifanya nizidi kupata nguvu ya kutafuta na kutojikwanza na kuwaona masikini ni wazembe wakutafuta.Ndevu amepewa mbuzi ww na mdogo na ng'ombe ametoswa na god hakumpa kitu gani.
 Asikwambie mtu bana kuna raha yake hapa ww ambae hujawahi kupitia maisha ya hali ya chini kma sisi huwezi jua,tuachie sisi watoto wa uswazi.
 Mamaaa mwenyewe akose tena anabana mpaka kivuli Wema Sepetu kaungana na mzee amakweli mapenzi msiingilie mtakuja kupata aibu siku moja hawa hapa tena sasa tazama picha inayofata nn Diamond anafanya ndio utaamini hawa wanataka tuamini picha ya jiko bakuli.
 Chukua fanta wema wangu weee hata kama ukiwa na mbili si mbaya ilimradi tu tunywe rangi zakkufanana.Diamond akimpa soda wema.
 Hapa imeshafika na Wema kaipokea sasa tuambieni huyo Jokate yupo wapi hapa?Waacheni bana watu wanaopendana wakiachana hata nyinyi hamtojua,mkijua mjue sio kweli mnazungushwa nyie vichwa vyenu tu wao wanago.
Mama Diamond na wadau wengine.
Picha kwa hisani ya Diamond mnyama thisisdiamond.com