Tuesday, October 9, 2012

VITU HIVI NDIO SABABU YA KC KUPEWA JINA LA BECKHAM WA FC KILIMANJARO

 Ukitazama hii picha wakati wa enzi zangu natumikia fc kilimanjaro ndio utapata picha kamili kwanini nilikua naitwa Beckham wa fc Kilimanjaro
 Ilikua lazima niulize kwa anaetaka mpira awekewe kichwani au kwenye mguu ili ushindi upatikane.
 Upokeaji na utoaji wangu wa pasi ulikua wa umakini sana kuakikisha fc Kilimanjaro inaelekea pazuri.
   Mipira yakulushwa na ile iliokufa yote ilikua ni jukumu langu .
    Nikijiandaa kupokea mpira tayari kwa kumfikishia mwingine.
 Nilichokua nafanya ni kuomba mpira upande wangu kisha naupeleka kati,hapa nikiwahi mpira unaoletwa na Abui Fuad yeye mwenzangu mpaka sasa anaitumikia fc Kilimanjaro.
     Tege la maana
 Hapa fc Kilimanjaro tukiwa katika chumba cha mapumziko.Jay jay,Kc,Omar na Shabani
Hapa nilikua na kaka Andrew huyu alishawahi kukipiga league ya bongo wakati huo na ndio miongoni mwa wachezaji waliokua wanaisaidia fc Kilimanjaro ushindi.Kwa sasa sisi wote ni wastaafu wa fc Kilimanjaro.