Tuesday, May 24, 2011

HVI KWELI HOME BOY WANGU UNATAKA KUUZA UHAI WAKO KWA BAISKELI?

 Unajua nilipotazama picha ya kwanza nikahisi kama jamaa namjua,nilipoendelea kutazama zaidi nikazidi kukubaliana na kichwa changu.Na niliposoma jina lake ndio uhakiki wangu ukatimia na kuanza kupatwa na huzuni mkubwa.Kwa ufupi jamaa namjua tunaishi nae mtaa kimoja temeke na alikua golikipa wetu mzuri sana mpira wa makalatasi kipindi wadogo.Sema bdae nilipokwenda bongo nikakuta ameanza kutumia madawa ya kulevya,nikajua mwisho wake unaweza kufikia huku siku moja.Mimi sina zaidi ya kusema kumuombea mungu ajijue yeye nani na anathamani gani kama binadam asiuchezee uhai wake.

 Dah tazama hapa wanavyomgombania kama mpira wa kona.

 Huyu askari na jamaa aliovaa shati jeupe ndio waliomnusuru la sivyo yangekua mengine.


 Jitambue ndugu yangu usije ukakukuta umauti wako kwa sababu ya vitu vidogo.

Hili guu la jamaa sidhani kama lilimkosa.Hili tukio lilitokea morogoro nadhani mjomba Jamil na Abui mtakua mnapajua haya maeneo.