Saturday, May 21, 2011

JAMANI EBU KUENI NA HURUMA KIDOGO MUMPISHE KTK KITI ASIJE KUANGUKA NA MTOTO.


Haya ndiyo maisha ya kawaida ya wakazi wa jijini Dar Es Salaam. Ambapo akina mama wajawazito ni nadra kupishwa kwenye viti vya daladala. Pichani ni jambo la kusikitisha ndani ya daladala moja kuona uonavyo.Jamani huu ni uungwana kweli?.....Picha hii imenikumbusha siku moja nilichukua daladala kutoka Ruhuwiko nikiwa na safari ya kufika Peramiho na mara kwenye daladala akaingi bibi mmoja na hakuna aliyenyanyuka kwenye kiti chake . ...isipokuwa mimi na wasafiri wengine wakaniambia kama daladala ile ni ya kwangu au nimepanda bila kulipa nauli?

Jibu langu lilikuwa kwamba nimejiona mimi mwenyewe ndani ya bibi huyu maana baada ya miaka kadhaa nitakuwa hivi na nitapenda kukua kwenye siti ....sijui kama walinielewa....Je wewe unaelewa ? Na je ungekuwa wewe upo ndani ya daladala na mamamjamzito, mama aliyebeba mtoto mgongoni bibi au babu wanaingia ndani ya daladala je ungempa siti yako?