Sunday, May 29, 2011

MIONGONI MWA MASHABIKI WA MANCHESTER AMBAO KIPIGO KILIWAHUSU.

 Pole sana ndugu mgiriki najua kipigo jana kimekufanya hata chakula kisipite.
 Huyu ndugu yangu Mweneu kiukweli mkiwa mnatazama mpira wala hujui kama anapenda Manchester au la ila jibu upatikana baada ya mechi kuisha na kupata ushindi,huwa na furaha sana ila jana alikumbwa na hasira mpaka akawa anatukana wachezaji hawachezi vile inavyotakiwa wewe ukipewa nafasi utacheza kaka?Pole sana ndugu yangu Mweneu ndo mpira jifute machozi na kombe la league ya england.
 Shekhan Rashid sijui jana ulikua katika hali gani maana manchester wakifungwa uzimaga simu vipi jana kaka?
 Mimi jana kiukweli kipigo hakikunistua sana sababu naujua mpira wa fainal una matokeo mawili na si matatu kufungwa au kufunga.Sema huyu jamaa wa katikati Herry najua jana yeye alikua na homa kali sana je ulimeza panadol kaka?kwa upande wa Cledo mwaipopo najua alikua na furaha yeye ni mzee wa bwawa la maini najua jana alikua Barchelona.

Hahahahaha huyu kipa wetu wa kutumainiwa wa kilimanjarofc hapa stockholm Kablau hua anaongea maneno yote Manchester wanaposhinda sasa jana ilikuaje ndugu?pole ndugu najua ulitamani ungedaka wewe jana ila Mesi popote anashinda.