Sunday, June 12, 2011

HAYA KAKA DIMOND UMESIKIA MANENO YA MWENZAKO HAYO HAPENDI TENA.

 Mhusika katika tasnia ya filamu za Kibongo, Wema Abraham Sepetu amefunguka kuwa, hakuna mwanaume aliyempa nafasi kubwa moyoni mwake kama muigizaji mwenzake, Steven Charles Kanumba, Risasi Mchanganyiko limejaza data kwenye mkoba.

Akizungumza na gazeti 5 Star Bongo, Risasi Mchanganyiko katika ‘spesho intavyu’ ndani ya hoteli ya kifahari ya The Atriums, Sinza ya Afrikasana, Dar es Salaam, Wema alisema kuwa, katika maisha yake ya kimapenzi, kati ya wanaume wote aliowahi kuwa nao, ni staa huyo pekee ndiye aliyempenda kupindukia.

Wema ambaye pia ni Miss Tanzania 2006/07 alisema kuwa, enzi za penzi lao alikuwa hawezi kuficha hisia zake kwa jamaa huyo hivyo kujikuta akimpa penzi lake lote.
“Mh! Siyo siri, kati ya wanaume niliowahi kuwa nao, Kanumba aliuteka moyo wangu kwa asilimia zote,” alisema Wema aliyefanya ‘wandazi’ katika Filamu ya The Diary na kuongeza: 

“Sidhani kama kuna mwanaume mwingine nitakayempenda kama Kanumba. Mbaya zaidi nafasi ya kumpenda mwanaume kama ilivyokuwa kwa Kanumba niliifuta tangu tulipotengana.”
Huku akionesha hisia, Wema aliendelea kutambaa na mistari: “Nilimpenda kiasi kwamba sikuamini kama angesababisha nilale gerezani Segerea kwa siku tatu. Nilimpigia magoti ili anisamehe lakini hakunielewa.

“Pamoja na hayo yote lakini bado tunasalimiana vizuri na kushirikiana kwenye kazi, kuhusu mapenzi, sidhani kama muda unaweza kurudi nyuma.
“Mama yangu aliwahi kuniambia katika maisha yangu kama nikimpa mtu moyo wangu wote halafu akanipeleka polisi, nimuepuke.
Mimi ni mwanamke so najua bado Kanumba ananipenda na hata nikimwambia turudiane hawezi kuchomoa.”

Ukimwacha Kanumba, Wema aliwahi kutajwa kutoka kimapenzi na mastaa wa Bongo Fleva, Herry Samir ‘Blu’, Khaleed Mohamed ‘TID’ bosi wa Hartmann Productions, Hartimann Mbilinyi, mwimbaji wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Charles Gabriel ‘Chalz Baba’ na huyu wa sasa ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul ‘Diamond’.Habari kwa hisani ya global publishers.