Tuesday, September 6, 2011

KWA WALE WALIOTAKA KUFIKA NYUMBANI KWETU FATA MAELEKEZO NITAKUFIKISHA.

 Watu wengi wamehitaji niwaelekeza nyumbani kwetu uswazi ninapofikia nikienda kwa mapumziko baada ya kazi ngumu za ulaya.Sasa twende pamoja na maelekezo haya.Nyosha hii balabala moja kwa moja hao washkaji usiwaulizie  maana wanatakaga pesa kukuelekeza au wakupoteze.
 Utakutana na hawa mama ntilie fanya kama uwaoni nyoosha sema kama utakua umeshikwa na njaa unaweza kusimama na kula kidogo sahani shilingi 300 lumbesa hata mimi nakulaga hapa nikifulia si unajua ukienda na pesa ambazo zinatoka tu lazma ziishe?
 Hawa jamaa wasubiri mpaka wapite maana ndio zao kuziba njia na matenga yao ya nyanya ila ndio wanaotupatia huduma maeneo yetu.Wakipita wewe endelea na safari karibu utafika nyumbani kwetu.
 Utakutana na hawa wazee wa kazi wakipakua choo si unajua tena huku kwetu gari la kunyonya hakuna njia ya kupitia tumejenga jenga tu.Na kutokana na hili eneo ukipita harufu inakua yakukatana na shoka ziba pua endelea na safari karibu unafika mdau.
 Utakutana na hichi choo kipite na usijaribu kutupia jicho maana inawezekana kuna mtu ukapewa kesi ya kuchungulia nyoosha moja kwa moja.
 Utakuta mfereji wa maji machafu si unajua huku kwetu hakuna mashimo ya chini kwa chini ya kupitisha maji machafu?Na chakushangaza watoto wanacheza hapo hapo sema usmind mdau tazama linalokuhusu endelea na safari.
Ukiwaona hawa wazungu wanaingia katika huu mgahawa kupata chips zege sasa anza kuhesabu nyumba ya 10 kutoka hapa utakua umefika nyumbani mdau,natumai sijakuchosha na safari ya kufika nyumbani kwetu.