Thursday, September 1, 2011

MWIZI ACHOMWA MOTO MTONI MTONGANI TEMEKE.

 Wananchi wenye asira wamshushia kipigo mwizi na baadae kumchoma moto mpaka kufa.Kwa upande mwingine inasikitisha sana kwa wananchi kuchukua sheria mikononi mwao wakati kuna vyombo vya sheria.Na pia kwa upande mwingine kibinaadamu unawezaje kua jasili kwa kutoa roho ya mwenzio kwa sababu ameiba simu au kuku unadhani thamani ya kidole chake tu ni sawa na simu yako au kuku wako?kama si hivyo iweje umfupishie uhai wake?kwakweli inasikitisha sana watu wanakua na roho za kinyama kama hivi.Mimi kwa mtazamo wangu wananchi wa Tanzania kwa hizi hasira zao wangekwenda kuwachoma wale mafisadi ambao wanaiba mabilioni ya wananchi yatokanayo na kodi ambayo ni jasho lako ww mwenyewe na alikusaidii,lakini matokeo yake unamchoma moto mwizi wa simu wakati haki yako kubwa kabisa unaibiwa na mafisadi wa nchi!!!.Huu ni mtazamo wangu.
Picha kwa hisani ya Ommy a.k.a baba Rahman.