Saturday, September 10, 2011

MV.SPICE ISLANDER YAZAMA NA KUUA IDADI KUBWA YA WATU

 Watu wasiopungua 187 wamekufa baada ya meli iliyokuwa imezidisha mizigo kuzama katika pwani ya kisiwa cha Zanzibar ikiwa na watu takriban 800.
Msemaji wa serikali amesema watu 620 walionusurika wameokolewa. Serikali imetangaza siku tatu za maombolezo.
Inadhaniwa kuwa meli hiyo ilizama baada ya injini yake kukosa nguvu.

Shughuli za uokoaji zilikwazwa kwa kuwa meli hiyo ilizama usiku.
Meli iliyozama

Zaidi ya watu 100 bado hawajulikani walipo, lakini watu 325 walionusurika wameokolewa, kwa mujibu wa waziri wa masuala ya dharura wa Zanzibar.
Meli hiyo, MV Spice Islander ilikuwa ikisafiri kati ya Kisiwa kikuu cha Unguja kuelekea Pemba.
Meli hiyo ilikuwa ikirejesha watu baada ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani.

Msaada

Mamlaka za huko zimezidiwa na tukio hilo na zimeomba msaada kutoka nje.
Serikali ya Zanzibar imeunda kituo cha uokoaji na kutoa wito kwa taasisi zote kusaidia katika shughuli za uokozi. Serikali hiyo pia imeomba msaada kutoka nchi nyingine za nje, kama vile Kenya na Afrika Kusini.
Walionusurika walichukuliwa na boti za kibinafsi na kupelekwa katika bandari ya Zanzibar, amekaririwa kamishna wa polisi wa Zanzibar Mussa Hamis.
 Miili ya watu imekuwa ikisukumwa katika pwani ya Zanzibar na mawimbi. Mpaka sasa miili ya watu 100 wamepatikana, amesema mwandishi wa BBC Ali Saleh akiwa Zanzibar.
Maelfu ya ndugu na jamaa wanasubiri kusikia taarifa za ndugu zao ambao walikuwa ndani ya meli hiyo, anasema mwandishi wetu.
Mohhamed Aboud, waziri wa masuala ya dharura wa Zanzibar anasema watu 259 walionusurika wameokolewa lakini 40 kati yao wamejeruhiwa sana.
Boti yetu imechelewa kwa sababu wanatumia vyombo vyote vya baharini kuokoa watu

Catherine Purvis, mtalii kutoka Uingereza aliyepo Zanzibar, akisubiri boti ya kwenda Dar es Salaam amesema ameshuhudia miili ya watu wengi ikitolewa ndani ya maji.
"Nimesimama katika bandari ya Zanzibar nikiwa na watalii wengine kama 10 wa Marekani na Uingereza.
"Boti yetu imechelewa kwa sababu wanatumia vyombo vyote vya baharini kuokoa watu".
Rubani mmoja wa helikopta Kapteni Neels van Eijk alipita juu ya eneo la tukio.
"Tuliona walionusurika wakiwa wameshikilia magodoro na majokofu au chochote kile kinachoweza kuelea. Ni vigumu kusema idadi kamili, lakini naweza kusema walikuwepo zaidi ya watu 200 walionusurika ndani ya maji na miili ya watu pia," ameiambia BBC.
 Wakati huo, kulikuwa na boti chache zilizofika katika eneo hilo. Walikuwa wakitafuta walionusurika, ingawa bahari haikuwa imechafuka sana, mawimbi walikuwa makubwa, kwa hiyo ilikuwa vugumu kuona walionusurika.
"Tulirusha ndege yetu na kuziongoza boti hadi kwa watu walionusurika ili waweze kuwachukua. Kulikuwa na miili kadhaa ndaniya maji."
Meli hiyo iliondoka Unguja takriban saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki na inadhaniwa kuwa ilizama majira ya saa saba usiku.
Ilikuwa imebeba abiria wengi kiasi kwamba baadhi ya abiria waligoma kupanda, amekaririwa abiria mmoja aliyenusurika Abdullah daid, akizungumza na shirika la habari la AP.
Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Kikwete na Raisi wa Zanzibar Dr Shein wakikagua miili ya watoto ambao imetokana na kuzama kwa meli hiyo.
Huu msiba ni wa taifa kwa ujumla,Kikubwa kumuomba mungu awastili mahala pema waliotangulia na awape nafuu majeruwi wote amen.