Monday, July 18, 2011

FC KILIMANJARO WASHINDWA KUTETEA KOMBE LAO MBELE YA LIBYA

 Walianza kucheza Maveterani dhidi ya Libya na Libya kuibuka na mshindi mkubwa sana.Na baadae Fc Kilimanjaro ilishuka dimbani kucheza nusu fainal yake dhidi ya Sierra Leone na ulikua mchezo mgumu sana,lakini mpaka mechi imekwisha Fc Kilimanjaro iliongoza kwa bao 3-1.Wakapata mapumziko kidogo kabla yakumalizia kwa kucheza Fainal dhidi ya Libya nayo ndio ilikua fainal ngumu kupata kutokea.Mpaka mpira unakwisha team zote zilitoshana nguvu kwa kufunganga 2-2 ndipo muamuzi akaongeza dakika na baada ya dakika za nyongeza kuisha bila goli yakafata matuta ndio hapo Fc kilimanjaro walipopoteza kombe lao ambalo wamelishikilia kwa karibu misimu 4.
 Wachezaji wakishow love kabla ya mechi



 Watu wakibadilishana mawazo kabla ya mechi
 Mtoto wa nyoka ni nyoka kipaji kinachomoza mapema


 Libya wakipasha misuli

 Team zote mbili zikiwa pamoja kuonyesha upendo mpira wa miguu sio vita.
 Capten wa Fc Kilimanjaro Maveterani akitoa maelekezo baada ya jahazi kuonekana kuzama


 Chedazzzzzzzz
 Maveterani wakijadili kipigo chao
 Kaka Mjengwa nae alikuja kuungana nasi katika kutazama Fainal hizo na kuchukua matukio kadhaa kwa ajili ya blog yake.

 Fc Kilimanjaro nayo iliingia uwanjani kucheza Nusu fainal yake.



 Mashabiki wa FC kilimanjaro

 Kilimanjaro Fc wakishangilia ushindi wao




 Niliungana na ndugu zangu katika kupata picha
 Fainal ilikua yakukatana na shoka
 Mapumziko
 Wakipangana nani aanze penati na nani amalize


 Libya walishangilia ushindi wao kwa furaha kubwa sana na hii imetokana na kutowahi kuwafunga Kilimanjaro misimu yote minne.
 Freddy Nice na Meneja Nyupi wakifarijiana baada ya kipigo na kupoteza kombe.
 Mgiriki akiwa ameshikilia kikombe cha mshindi wa pili.
 Baada ya mechi watu walipata chakula na vinywaji vilivyoandaliwa na Kilimanjaro