MSHAMBULIAJI wa timu ya Azam Fc ya jijini Dar es Salaam, Mrisho Ngasa, amefuzu majaribio yake ya kuichezea timu ya Seattle Sounders ya Marekani inayoshiriki Ligin Kuu ya England.
Ngasa aliondoka jijini kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya kufanya majaribio na timu hiyo iliyofika dau la kumnyakua kwa ajili ya kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
Aidha baada ya kuwasili nchini Marekani Ngasa alifanyiwa majaribio ya kwanza katika mchezo wa kirafiki baina ya timu hiyo na Manchester United ya Englandm, ambapo Ngasa alichezeshwa dakika 15 za mchezo huo na kuwaacha hoi mashabiki lukuki waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.
Pamoja na jitihada za Ngasa alizoweza kuonyesha katika dadkika hizo 15 na kukosa bao katika dakika za mwisho za mchezo huo, lakini timu yake ilibugizwa mabao 7-0.
Akithibitisha habari hizi kwa njia ya sim, Meneje wa Azam Fc, amesema kuwa baada ya Ngasa kufanikiwa kufuzu majaribio hayo, sasa kinachofuata ni utaratibu wa uhamisho wa mchezaji huyo ili aweze kuitumikia vyema timu yake hiyo mpya.
Aidha, kiongozi huyo akisema kuwa kutokana na Ngasa kufuzu kucheza soka la kulipwa, sasa timu hiyo inajipanga kutafuta mchezaji atakayekava nafasi yake, huku wakijiandaa kuingia mkataba wa kumuhamisha Ngasa ikiwa ni pamoja na dau kamili ambalo bado hadi sasa halijawekwa wazi.
Habari kwa hisani ya mateja 20.