Ndugu zangu ebu mtazameni mwanadam mwenzetu huyu mungu alivyomuumba.Vipi wewe mungu ajakupa kasolo yeyote katika mwili wako unashindwa kumshukuru kwa nguvu zako zote?Maana kuna binadam wengine kunyimwa kipato au kitu flani cha maendeleo wanafikia hatua hata yakumkosoa mungu kwa kukunyima kazi nzuri,maisha mazuri na vinginevyo vya dunia.Wakati huyu mwenzetu na wazazi wake wanakesha kwa kumuomba mungu aonyeshe miujiza yake ili mtoto wao awe kama wengine,naimani kabisa hawamuombi mungu wapate utajili wao kwa muda huu wanaomba hali ya mtoto wao iwe kama binadam wa kawaida.Lakini sisi wengine mungu katupa viungo sawa bila kasolo yeyote na tunashindwa kumshukuru au unakosa raha na mawazo kila kukicha kwa kukosa vitu vidogo vyaduniani.Sasa jiulize huyu na wazazi wake wanamshukuru mungu kwa huu mtihani aliowapa vipi wewe umepewa mtihani wa duniani na maisha unshindwa kumshukuru?
Kijana huyu mwenye miaka 10 anaeishi Bangladesh amezaliwa akiwa hivi,na madaktari wamesema kwa usalama wa kijana huyu inabidi aachwe hivi kama atafanyiwa upasuaji wowote unaweza kumsababishia kifo.