Sunday, July 3, 2011

KISOMO CHA KUMUOMBEA MAREHEMU MAMA YAKE ALLY






 Shekh Butoi alituongoza katika dua nzima yakuombea mama yetu mpendwa mungu amlaze pema peponi amen.

 Mtoto wa marehem Ally akimuwekea ubani mama yake mpendwa Inshallah dua zetu zimfikie amen.

 Balozi nae alijumuika nasi tunafarijika sana kuona kiongozi wetu anakua na sisi bega kwa beka kwa raha na shida mungu akupe heri ktk uongozi wako amen.
 Kaka said akiwa na Dada kabwe jikoni kuakikisha mambo ya sadaka yanakwenda sawa.
 Watu waliitikia wito kwa wingi inapendeza na hata mwenzetu kajisikia kama amejaliwa ktk kipindi hiki kigumu.



 Mzee wetu mlezi Awale pia alijumuika
 Mashekh wengi siku ya leo walijitokeza











 Nayla nae alijitokeza katika dua na baba yake.

 Mfiwa akiwa na ndugu zake waliokuja kumpa pole Lilian,Linda na Nasra pia tunawashukuru sana katika swala la chakula kwani wao ndio wapishi wakuu
 Nikibadilishana mawazo na dada zangu baada ya dua
 Dada Linda mpishi mkuu wa chakula cha kisomo chetu akiwa ktk pozi baada ya shughuli kuisha shukrani kwako nyingi.
 Shukrani kwenu akina mama pia peke yetu bila nyie ingekua ngumu sana kufanikisha kusudio letu mungu atawalipa.


 Dada Lilian toka jana tulishilikiana nae ktk Kuandaa shughuli yetu kwakweli mungu akulipe amen.
 Skukrani kwenu pia dada Lilian na Dada Kabwe ktk kutuwekea sawa chakula  mungu atawalipa amen

Ama kwa hakika tumeonyesha ushilikiano mkubwa kwa wale wote waliotokea na hata wasiotokea kwa kubanwa na majukumu.Inapendeza na tushikamane hivi hivi kwa kila jambo.
Na mfiwa kaka Ally kanituma kuwafikishia shukrani zake kwa wote walioshilikiana nae ktk kumfariji kwa namna moja au nyingine,anasema ana chakuwalipa yeye kwani mlichomfanyia ni kikubwa hata awape nini afikii gharama yake zaidi anawaombea tu kwa mungu yeye ndio atakulipeni.