Thursday, August 25, 2011

AMEKOSA NINI MALAIKA WA MUNGU HUYU MPAKA ATUPWE?

 Masikini malaika wa mungu amekosewa nini mpaka afupishiwe maisha yake?tena ni msafi hana hata kosa moja katika hii dunia.Naimani mwenyezi mungu atamuadhibu anayehusika.Kitoto kichanga kilikutwa kimetupwa katika mto na tayari ameshakufa.Kiukweli nilipokutana na habari hii mwili wangu ulisisimka sana na kujiuliza maswali mengi bila majibu juu ya tukio hili.Ila swali la mwisho ambalo ndio jibu nimekosa kabisa ikiwa wewe mwenyewe umekutana na mwanaume kwa raha zako na ukashika mimba miezi 9 jumlisha uchungu wa kuzaa kweli kabisa unamtupa mwanao uliompatia tabu?Kama maisha magumu huwezi kumuhudumia kwanini usiombe msaada kwa wasamalia wema?Hvi unadhani wanawake wenzake wale ambao mungu ajawajaalia kupata mtoto wala mimba kwa bahati mbaya wanamlaani vipi mwanamke aliofanya kitendo hichi cha kinyama?
Watu wakishuhudia tukio la kuokotwa kwa mtoto mchanga alietupwa katika mto na kukutwa amefariki.