Saturday, August 13, 2011

BAADA YA FTARI KAMERA YA BLOG MTAANI

 Baada ya ftari nikaona ninyooshe miguu kuweka sawa vitu vilivyomo ndani ya tumbo langu ndio nikapitia kazini kwa kaka yangu a.k.a mjomba wa munich.Kazini kwa kaka Mjerumani pale tulipata vinywaji vyepesi na yeye ndio alikua mdhamini mkuu alitugharamia mimi na kaka Khamis.
 Kaka Khamis akishow lv
 Mjerumani akiwa kazini huku akipiga stori na sisi za hapa na pale
 Kaka Khamis kiukweli huyu mtu mara nyingi huwa tunakutana na kusalimiana juu juu tu lakini jana kuliongozana pamoja katikati ya jiji la Stockholm na tukazungumza mengi kiukweli nilipata faida kubwa sana sijui kama yeye amelitambua hilo.Ikafikia mpaka hatua ya kubadilishana namba hii inamaana kwamba kila mtu alimuona mwenzie anamfaa kwa namna moja au nyingine katika harakati za maisha na hii inazidi kunifundisha nisimdharau yeyote bila kujali uwezo wake au umaskini wake unaweza kupata faida kubwa.Asante kaka Khamis.