Monday, August 15, 2011

FABREGAS:POLENI SANA MASHABIKI WANGU WA ARSENAL NAJUA IMEWAUMA


Masaa machache tangu ajiunge rasmi na Barcelona, Cesc Fabregas amewaomba radhi mashabiki wa klabu ya Arsenal kwa kutowaambia lolote juu ya uhamisho wake kwenda Barcelona huku akiahaidi kuwapa sababu zilizomfanya ahame kwenye klabu ndani ya siku chache zijazo.

Fabregas ambaye alikuwa nahodha wa Arsenal amerudi Barca baada ya kuwepo Emirate kwa takribani miaka 8 na hatimaye jana Jumatatu alimaliza utata wa uhamisho wake kwenda Catalunya.

Kiungo huyo Spain anasema uongozi wa Arsenal waliweka sheria kali juu ya kuongelea uhamisho wake na ndio maana alishindwa kuzungumza chochote.

Fabregas anakiri ulikuwa ni uamuzi mgumu kuondoka Emirates Stadium na anasema atawaambia mashabiki wa Gunners ukweli wote kuhusu uhamisho wake wa kujiunga na Barca.

“Nina muda wa kuzungumza juu ya suala hili na uhakika nitafanya interview maalum kwa ajili ya kuwaambia story yote mashabiki wa Arsenal kuhusu uhamisho wangu.

“Samahani sikuweza kusema chochote katika kipindi chote cha miezi miwili na nusu, Arsenal walinikataza kuzungumza lolote kuhusu uhamisho wangu hata kama nilikuwa nataka kufanya hivyo lakini nilishindwa.

“Sijisikii vizuri na nilikosa amani juu ya hili kwa sababu nilikuwa na mahusiano mazuri sana na mashabiki kwa miaka mingi.Ilinichukua muda mrefu kupata sapoti na imani kwangu yao na inaniuma kwamba naweza kuwapoteza wao na sapoti zao kwangu.

“Maneno pekee niliyonayo na shukrani kwao, sitosahau vyote walivyonifanyia, nilifanya na kujitoa kwa kila kitu kwa ajili klabu ile na najua kwamba wanafahamu lakini najua kwamba ni uamuzi sahihi kurudi hapa(Barcelona).

“Ninaomba radhi kwa fans kwamba sikuwaabia chochote.Nina masikito makubwa kuondoka.Nimetumia robo tatu ya maisha yangu pale, miaka 8, nina huzuni mkubwa lakini maisha yanaendelea.” -Fabregas
Kwa hisani ya shaffih dauda.