Tuesday, August 9, 2011

KAMA UNAELEKEKEA BONGO MAPUMZIKO BEBA DUMU LAKO LA MAFUTA KWA AJILI YA GARI AU PIKI PIKI YAKO.

Hvi jamani hii inchi yetu inaelekea wapi?na viongozi wapo wapi?na je viongozi wetu wa nchi pia tabu hii yakugombania mafuta ianawakuta au sisi tu wa hali ya chini?Kiukweli inasikitisha sana maana hata swala la umeme halijaisha limekuja hili la mafuta hivi tunaipeleka wapi nchi yetu?inafikia muda mtu unaichukia nchi yako kwa upuuzi wa watu wachache kabisa ambao wao na familia zao wamekaa ktk viti wanatazama luninga huku wakicheka.Na je vipi yule ambae mzalendo au mgeni akiona mambo kama haya atashawishika kuwekeza katika nchi kama hii?
Kiukweli maswali mengi watanzania tunayo na majibu hatuna na sidhani kama kuna wakutujibu.