Friday, August 12, 2011

LEO TULIKARIBISHWA KATIKA FTARI NA HAMIS ABUI,A.K.A BABA NAYLA

 Kiukweli leo mtoto hakutumwa dukani kitu cha kupiga goti hata hujui uanze wapi na uishie wapi.

 Wakongwe wote wa jiji la Stockholm waliudhulia kama uonavyo.


 Hapa walikutana wachezaji wa zamani wa Moro United Jamil na Aliekua capteni wake Hamis Abui wakati huo golini alikua anadaka Juma kaseja.


 Baada ya ftari tulipeana mawili matatu yakukumbushana juu ya umuhimu wa funga katika mwezi wa mtukufu.
 Picha ya pamoja

 Ahmed Dady akizungumza mawili matatu kutoka kwa mlezi wa vijana wa Stockholm mzee Hawale.
 Mtupia nyavu nae alikuwepo hapa akiagana na Mzee Hawale,kiukweli usiofichika huyu mzee kwa upande wangu mimi namuheshim zaidi ya mzazi wangu kwani anamaana kubwa sana katika maisha yangu mimi kama K.Karama sina yakuongea mengi juu yke ila namuombea dua nyingi sana kwa roho yake safi ambayo sijui nimfananishe na nani.Mwenyezi mungu akuzidishie mzee Hawale kwa kila jema kwa baraka za mwezi huu amen.
Tunashukuru sana Baba Nayla kwa kutukutanisha kwa pamoja siku ya leo kupata ftari.Mimi kwa upande wangu natoa shukrani kubwa sna kwani si jambo dogo ulilolifanya,mbali na kufturu pia umetuunganisha kwa usiku wa leo kwani kila mtu anamajuku yke ila tumekutana na kubadilishana mawili matatu na kufurahia kwa pamoja.Asante sana kubwa ni dua tu nyingi zikufikie wewe na familia yako kwa ujumla na mungu awape malipo makubwa kwa hilo mlilolifanya amen.