Saturday, August 11, 2012

JOKATE AFUNGUKA JUU YA HASHEEM THABIT


WAKATI ikidaiwa kuwa yupo kwenye mahusiano na watu maarufu kwa kimya kimya kimwana Jokate mwegelo, amepasua jipya na kudai kuwa aliwahi kutoka kimapenizi na mcheza kikapu maarufu Hasheem Thabeet lakini hakudumu kutokana na sababu mbalimbali.

Ikidaiwa kutoka kimapenzi na mchezaji huyo maarufu wa kikapu anayekipiga nchini Marekani, ni baada ya jina lake kuwa kubwa pamoja na umaarufu wa fedha ndiyo ulimfanya kimwana huyo kuvutiwa.

Jokate alidakwa na DarTalk ili kueleza namna anavyoandamwa na stori za kuwa amekuwa kwenye mahusiano na watu kimya kimya ambapo idadi yao inaweza kuwa kubwa, ambapo alidai kuwa suala lake la mahusiano hakuna mtu linayemuhusu kwani yenye si kama wasanii wa bongo muvi.
Aliongeza kuwa alikuwa kimapenzi na Hasheem lakini haimanishi kuwa kutokudumu kwao kulitokanaa na habari kuwa yenye ni ‘gold digger’ hapana, bali ni sababu ambazo hakutaka kuziweka wazi.

Alidai kuwa mara nyingi maneno yamekuwa yakisikika kwa watu hata kwenye mitandao lakini haoni kama kuna umuhimu wowote wa kujibu kwani haitaji kupoteza muda wa kujibizana na watu wasio na faida yoyote kwake.

Jokate ambaye ni mmiliki wa fashion brand ya Kidoti Lovingamekuwa akihusishwa na kutoka kimapenzi na msanii Diamondkimya kimya ambapo pia kuhusu hilo, alikanusha na kudai kuwa wao ni marafiki na hakuna chochote kinachoendelea, ingawa alidai kama binadamu hakuna kinachoshindikana wao kuwa wapenzi kwani wote wanapendana.