Wednesday, August 22, 2012

WASWAHILI WANAKWAMBIA MKATAA KWAO MTUMWA.NIKIENDA MAPUMZIKO BONGO UTANIPATA KATIKA UWANJA HUU MUDA WA MAZOEZI

    Hapa ni maeneo ya tmk qwad huu ndio uwanja naoutumia pindi nikirudi  home kwa mapumziko baada ya kazi ngumu ya mwaka mzima ulaya.
 Kiukweli huu uwanja umetoa wachezaji wengi sana ambao waliopata kutamba league kuu na mpaka sasa bado unatoa wachezaji.Hapa kipindi hicho utampata Ramadhani Renny,Edwady Chumila wote marehememu kipindi hicho sisi watoto.Kuna Rashid Mlage wa Kabange,Hassani Banyai na wengineo.
 Hii hapa damu changa anakwenda kama Faki,huu ni mzao wa akina Adam Kingwande ambae yupo league kuu na Ramadhani chombo a.k.a Redondo wote walipitia pale kwa Aluko.


   Raha ya uwanja huu ni kuoga vumbi si kwa wachezaji,watazamaji mpaka wapita njia na hua hatunywi maziwa na hakuna anaeumwa kwa hilo tumeshajizoelea wenyewe.


   Hassani Banyai mkongwe na ndio kocha wa tmk Sqwad kwa sasa baada ya kujiuzulu ukocha Moro united.
     Hapa kati mwenye mpira  Haji Harambe dogo mbishi sana akiwa uwanjani vitu anavyofanya tofauti na umri wake.
     Mmadi a.k.a bosi chunda hawa miongoni mwa wakongwe wa tmk sqwad
     Muda mwingine kama hivi mikokoteni nayo inakatiza uwanjani nasisi tunasongesha kama kawa.
     Hapa Mabruki na Haji sijui kama hatampita huyu mtu angalia picha ya chini.
     Mwisho wake ukaishia hapo.
     Kipa wetu Teacher
     Hamza Kilaya enzi zake ilikua usumbufu mkubwa ila kwa sasa anapunguza tu mwili.

     Hili hapa jukwaa letu na ndio benchi la team pinzani la vijana maana hapa huwa mazoezi yanakua ya vijana na watu wazima,Mimi hua katika watu wazima wadau.
      Simon a.k.a whats up

     Hassani Banyai akiwa amepumzika kumpisha mwingine andeleze libeneke.