Thursday, August 30, 2012

MAMA NA MTOTO WAKE WAISHI MAISHA YA MKE NA MUME MIAKA 10 BAADA YA BABA KUFARIKI.

 Umati wa watu uliofurika kwa Mganga wa Jadi Flora Ndembo Namabengo wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma watu wapatao 400 wameomba Serikali ichukue Mkondo wa Sheria pia Mtoto wa Pili wa Mama Kondrada Ngonyani ameomba Serikali ichukue hatua za kisheria dhidi ya condorada ngonyani na joseph Mapunda.

Joseph Mapunda mwenye umuri wa miaka 40 amesema ameweza kuishi kindoa na Mama yake Mzazi Condorada Ngonyani 70 baada ya yeye kukubaliana wenyewe yeye na mama yake mzazi kuishi kindoa kama mume na mke alipo ulizwa Mama alikiri kuwa kweli wameishi kindoa kwa miaka 10 na anampenda Mume wake ambaye ni Mtoto wake Joseph Mapunda.
 Mama Condorada Ngonyani mwenye umuri wa miaka 70 ambaye ana ishi kinyumba na mtoto wake watatu wa kumzaa mwenyewe kama Mke na Mume hapo anaonekana akisononeka kwa nini jamii iingilie ndoa yake.
 Kwa mkoa wa Ruvuma hii ni mara ya kwanza mtoto wa kiume Joseph Mapunda pichani hapo juu kutembea na mama yake mzazi. Wana Ruvuma wanauliza tume jikwaa wapi watanzani hadi kupoteza mila desturi na maadili ya mtanzania pia kukiuka sheria za dini
 Joseph Mapunda ana sema upendo ni upendo amempenda mama na anaishi kindoa wamependana nyie watu mnataka nini kwetu?
 Mama Condorada Ngonyani anasema mara baada ya kufariki mume wake Mzee Mapunda alimchagua mtoto wake amrithi baba yake
Mh kiukweli hapa si sahihi kabisa na wametokota.Sijui nini kimewasibu ni mila au masharti ya waganga wao au sijui nini.Mimi nadhani sheria inabidi ichukue mkondo wake ili iwe fundisho.
Asante Adam Nindi wa ruvuma.